Picha hii iko HAPA
Kwa
muda mrefu kumekuwa na mjadala mkali kuhusu nguvu za mionzi ya
mnunurisho inayotolewa na simu za mkononi kama zinaweza kusababisha
kansa ya ubongo ama la. Hatimaye Shirika la Afya Duniani
limetoa tamko kuhusu utafiti unaoonyesha kwamba simu za mkononi
zinaweza kuwa zinasababisha kansa ya ubongo. Hatari hii inasemekana kuwa
ni kubwa zaidi kwa watoto wadogo na matineja kwani mafuvu yao bado
hayajakomaa sawasawa...
Naomba hii isiwe kweli kwani kama tunavyojua, Afrika ndiyo jalala la bidhaa feki, mbovu na zilizoisha muda wake.
Bila shaka nitakuwa sahihi nikisema kwamba simu zinazotoa mionzi
hatarishi kwa binadamu na zitakazokuwa zimepigwa marufuku sehemu zingine
za dunia ndizo zitarundikana Afrika.
Kama
utafiti huu ni wa kweli basi miongo kadhaa tu ijayo Afrika itakumbwa na
mripuko wa kansa ya ubongo – mojawapo ya kansa hatari kabisa na
inayohitaji tiba ghali sana!
Tunachoweza
kufanya kwa sasa ni kufuata mapendekezo yaliyotolewa yakiwemo kununua
simu zisizotoa mionzi mikali zaidi, kuweka simu mbali na sikio wakati wa
maongezi na kwa wenye uwezo kununua vifaa vinavyosafirisha mawimbi ya
sauti kama “Bluetooth”.
Vifaa hivi huwekwa sikioni na vinaweza kudaka mawimbi ya sauti ya simu
iliyowekwa mfukoni au sehemu nyingine na kuyasafirisha sikioni kwa
msikilizaji bila madhara yo yote.
Aina mojawapo ya kifaa cha bluetooth


0 comments:
Post a Comment