Kubalehe ni ule muda ambao mtoto wa kiume na wa kike anabadilika mwilini akielekea kuwa mwanadamu mwenye uwezo wa kuzaa.
Muda
wa kubalehe ni muda ambao kunakuwa na mabadiliko kwenye mwili wa
msichana au mvulana kumfanya awe mwanadamu mwenye uwezo wa kuzaa. Muda
wa kubalehe yaani muda wa mabadiliko kwenye mwili wa msichana na mvulana
ili kumfanya awe na uwezo wa kuzaa, huanza mapema kwa wasichana wakiwa
na umri wa miaka kama kumi na kuisha wakiwa na miaka kama 14 mpaka 16.
Wavulana huchelewa kidogo na huanza miaka 12 na kuisha wakifikia
miaka 18. Haya ni makisio tu ya miaka maana huenda kubalehe kukaanza mapema zaidi na kuchelewa kuisha.
miaka 18. Haya ni makisio tu ya miaka maana huenda kubalehe kukaanza mapema zaidi na kuchelewa kuisha.
Kwa wasichana dalili kuwa wapo kwenye huu umri wa kubalehe, maziwa yanaanza kuwa makubwa, nywele zinaota sehemu za siri na kwenye
makwapa; wanakuwa na chunusi na baadaye wanavunja ungo yaani wanapata
damu ya mwezi ya kwanza. Wavulana wanaota nywele vile kwenye sehemu za
siri na kwenye makwapa, wanaota ndevu, viungo vyao vya kiume yaani
korodani na uume vinakua, musuli inakuwa mikubwa na sauti inakuwa nzito.
Wakati
wa kubalehe vile vile ni wakati wa kuongeza kasi ya kukua haraka haraka
na kurefuka. Wanakua haraka kwa miaka kama mitatu hivyo baada ya
kubalehe wanakuwa wameishafikisha karibu na urefu wao wa utu uzima.
![]() |
Msichana anayeanzabalehe
|
Wakati wa
kubalehe mtoto anajisikia kuwa angependa kuwa na uhuru zaidi,
hujiangalia zaidi kimwili akiona jinsi anavyobadilika, huangalia mavazi
anayovaa kujiweka katika hali ya kwenda na wakati na mavazi wanayovaa
wenzake wa umri huo, wanaweza zaidi kuwasikiliza vijana wakubwa na hata kukopi tabia, matendo na mavazi yao.
![]() |
watoto ambao hawajabalehe
|
Pamoja
na kukopi, kuwasikiliza na kuwadodosa wakubwa zao, wakati wa kubalehe
mtoto anaendeleza uwezo na kipaji chake cha kutambua mema na mabaya. Ni
wakati ambao mtoto anahitaji ukaribu na misaada ya wazazi na ya wale
anaoishi karibu naye kumwezesha kujenga tabia nzuri ya kumsaidia
maishani na katika utu uzima.
Tunakaribisha maswali na mawazo kuhusu kubalehe kutoka kwa vijana na wazazi. Mwandikie Mhariri afyatele@gmail.com au andika na kutuma katika kiboksi cha maoni.
0 comments:
Post a Comment