-

-

-

-

-

Habari Mpya

Tuesday 29 July 2014

WANAOTUMIA UGORO WAKO HATARINI KUPATA SARATANI YA KINYWA

Maelfu ya wanafunzi wako hatarini kupata saratani za vinywa (Oral cancers) kutokana na kuongezeka kwa matumizi holela ya Ugoro (Snuff), Ongezeko la matumizi ya ugoro linakuja baada ya Wizara ya afya na ustawi wa jamii kupiga marufuku uuzaji wa Kuberi.

Akiongea na Daily news, mkuu wa kitengo cha afya ya akili na madawa ya kulevya wizarani, Dk norman Sabuni alisema kwamba kutokana na uchunguzi walioufanywa ulibaini kwamba matumizi ya ugoro yameongezeka na wasambazaji wakuu wakiwa ni walinzi wa Kimasai.
Alisema kwamba “tunajua idadi ya shule ambazo zimawafukuza walinzi wa kimasai baada ya kugundua kwamba wamekuwa wakiuza Tumbaku kwa wanafunzi. Tumbaku ni halali nchini hivyo tunachokifanya ni mwendelezo wa kuwaonya watu juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku”.

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi aliliambia gazeti hilo kwamba hana  taarifa kama kuna wanafunzi wanaotumia Ugoro na kuapa kwamba iwapo taarifa zitafika mezani kwake basi atachukua hatua stahiki.

Dk Sabuni alithibitisha kwamba wanafunzi wengi wanapendelea ugoro kuliko sigara kwasababu ugoro hauachi harufu baada ya kuutumia na unalewesha haraka ukilinganisha na Sigara. Aliongeza kwamba wanafunzi wengi hawautumii ugoro kwa kuuvuta kupitia pua kwakuwa wanaogopa kupiga chafya hivyo hutumia njia ya kinywa hali ambayo huwapelekea kulewa mapema kutokana na kiasi kikubwa cha ugoro kuingia kwenye mzunguko wa damu kwa kutuama kwenye lips za ndani ya domo.

Mtaalamu huyo alisema Matumizi ya Ugoro yanaweza kupelekea Saratani za lips, mdomo, koo, ulimi na hata kuathirika mfumo wa akili (mental disorders).

Muuzaji ugoro wa kimasai wa Mwenge aliliambia gazeti hilo kwamba sio kazi yao kujua mnunuaji yupi ni mwanafunzi na yupi sio mwanafunzi kwasababu wanunuzi huwa hawavai sare za shule wanapoenda kununua. Aliongeza kwamba, licha ya kuona kuwa watumiaji wengi ni vijana wadogo lakini pia amegundua kwamba watu kutoka mikoa mingine wamekuwa wakitumia Ugoro kwa wingi ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ni wamasai pekee ndio waliokuwa wameteka matumizi hayo.

Mudi Chokora (20), mtumiaji wa Ugoro kwa miaka mingi alililiambia gazeti hilo kwama mapenzi yake kwenye Ugoro yalianza kwa kuonja kwa walinzi wa kimasai waliokuwa wanaishi jirani na baada ya kipindi kifupi akajikuta amezamia kwenye matumizi ya Ugoro. Aliongeza kwamba ukilinganisha na Sigara ambazo gharama zake hupanda kila mwaka, Ugoro sio tu gharama nafuu lakini pia haihitaji kupiga mswaki mara kwa mara kwa kuwaogopa kushtukiwa na wazazi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

3 comments:

  1. I ope itakua bora zaid endapo utatachukua fursa yakuelimisha jamii kwa kina zaid athari ipatikanayo kwa matumizi mabaya ya ugoro mbali na faida zake mkuu

    ReplyDelete
  2. Asante kwa ushauri wako dokta ila Ni asilimi nyingi sana wanatumia ugoro da ee mola tuepushe na vishawishi hivi

    ReplyDelete
  3. Wataalamu wanaonekana kutojua sana juu ugoro na athari zake, ukubwa wa tatizo. Wasome wawe na majibu yanayolingana na nafasi zao.

    ReplyDelete

Item Reviewed: WANAOTUMIA UGORO WAKO HATARINI KUPATA SARATANI YA KINYWA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top