-

-

-

-

-

Habari Mpya

Monday 13 October 2014

matatizo kwa wadada katika sehemu zao za siri...

"Mimi ni mwanamke wa miaka 28 nimeolewa na nina 2 beautiful kids. Tatizo langu ni kuwa, toka nimezaa mtoto wa kwanza miaka 12 iliyopita huku kwenye Uke kunatoka udenda mweupe unanuka sana hata kama nikimaliza kuoga najiingiza vidole kujisafisha lakini harufu ipo pale pale na nikikaa na mtu karibu nahisi kabisa wanaisikia harufu yangu.


Mume wangu huwa namuuliza unasikia harufu huwa anasema hunuki hata kidogo ila naona anaogopa kuniambia labda nitakasirika huwa naona aibu sana kulala na mume wangu maana ni harufu kali mda wote lazima nivae pad la sivyo chupi yote inakua mbichi pia wakati wa kufanya mapenzi najaa sana maji hadi sijisikii kufanya na mume wangu pia nahisi labda na magonjwa sijui nifanye nini yani sina raha .... 
(Admin; Unaweza kuipost hii ili kama kuna mtu alishawahi kupata tiba anisaidie) thanks."
Jawabu: Ewe mdada wa miaka 28, kwanza pole na tunatoa shukrani kwa ufafanuzi. Ingekuwa ute mweupe mzito kama "cream" au laini kama "Lotion" (inategemea na mzunguuko wako kwa wakati huo) ningesema ni Utoko lakini "udenda" mweupe na wenye harufu ni wazi kuwa baada ya kujifungua ulipata maambukizo.

Kwakweli hapa nakushauri ukamuone Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa ushauri na hatimae matibabu, huenda tatizo halipo kwenye uke bali ndani kabisa kwenye viungo vya uzazi. Tafadhali fanya mihadi na Mtaalamu wa magonjwa ya akinamama, hasa wazazi kwa ushauri zaidi.

Ikigundulika unatatizo basi ni vema kama utamshauri mumeo pia apate matibabu kwani asipopata matibabu atakuambukiza tena kile alichonacho ambacho amekuwa akikutana nacho kila mnapofanya mapenzi.


Kumbuka kuwa wanawake huwa wana vijidudu marafiki ambavyo vinaishi ndani ya Uke lakini vikikanganywa kidogo kutokana na mabadiliko ya mwili wako, madawa, lishe n.k. vinaweza kukasirika na kusababisha ugonjwa maeneo hayo.


Vilevile kuna magonjwa mengine ya zinaa mtu anakuwa nayo kwa muda mrefu bila dalili yeyote na baadae ndio unakutana na matatizo kama hayo ya harufu, kuumwa tumbo n.k. Ni vema tukawa na tabia ya kupima magonjwa ya zinaa mara kwa mara kwani mengine hujitokeza yenyewe tu kutokana na "friendly bacteria" ambao kama nilivyosema wanawake wanavyo, wasipokuwa makini na "life style" au usafi wanaweza kuambukiza wenza wao.


Tunashauriwa mara chache wanandoa kutumia Condoms na kuangalia magonjwa ya zinaa mara kwa mara.....tendo la Ngono (yaani ile Uke kukutana na Umme) inaweza kusababisha mkanganyano wa wadudu marafiki wa ukeni na kuibua gonjwa la zinaa.

Kila la kheri huko kwa Dokta!!!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: matatizo kwa wadada katika sehemu zao za siri... Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top