-

-

-

-

-

Habari Mpya

Saturday 25 October 2014

NAMNA YA KUPAMBANA NA HARUFU MBAYA MDOMONII

Na Beatrice Githiri-HLH

Afya na usafi wa kinywa chetu ni muhimu ili kuboresha mwonekano wetu na pia kutufanya tujiamini. Harufu mbaya mdomoni hutufanya tusijiamini na pia kutunyima raha ya kucheka au kuongea mbele ya watu.

Harufu mbaya mdomoni husababishwana:
  • Bacteria mdomoni
  • Mdomo kuwa mkavu
  • Aina fulani za chakula

leo nitazungumzia njia kadhaa ambazo zinaweza kusaidia kuondoa au kupunguza harufu mbaya mdomoni. Endapo hizi njia hazisaidii ni vizuri kumwona daktari wa meno kwa ushauri na iba zaidi.

    Piga mswaki baada ya kula Usafi wa kinywandio namna nzuri zaidi kupambanana harufu mbaya mdomoni.
    Safisha ulimi
    Unapo swaki ni muhimu kusugua ulimi kwa kutumia mswaki ili kuondoa bakteria, mabaki ya chakula na’seli’ zilizokufa.

 Tafuna bubblish/Big G ambazo hazina sukari
Kwa kutafuna bubblish mtiririko wa mate huwa mzuri na hivyo kuondoa au kuafisha bakteria, mabaki ya chakula  na piahuzuia mdomokuwa mkavu.
Sukutua mdomo mara kwa mara
Kusukutua mara kwa mara huimarisha usafi wa kinywa na pia kuzuia mdomo kuwa mkavu, hivyo kuepusha harufu mbaya kutoka mdomoni.
Epuka uvutaji wa sigara
Uvutaji wa sigara hufanya mdomo kuwa mkavu na hivyo kusababisha harufu mbayakutoka kinywani.
Epuka au punguzavyakula vinavyosababisha harufu mbaya mdomoni
Vyakula kama vitunguu maji, vitunguu swaumu, samaki, mayai, kabeji, maziwa husababisha harufu mbaya. Pia vinywaji kama kahawa na pombe huleta harufu  mbaya haswa kwa watu wenye mtatizo ya kunuka mdomoni.


Ni matumaini yangu kuwa somo la leo limekupa ufahamu katika kuboresha afya ya kinywa chako kwa kuzuia harufu mbaya.

Kiafya tunashauriwa kumwona daktari wa meno kila mwaka na kama kuna matatizo, angalau miezi mitatu hadi sita.
Ijue afya ya kinywa chako kwa kwenda katika huduma ya kinywa na mdomo. Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ina kitengo cha meno na huduma hiyo inapatikana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: NAMNA YA KUPAMBANA NA HARUFU MBAYA MDOMONII Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top