Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na kutangazwa na Shirika la Afya Duniani WHO katika mkutano wake wa tarehe 19-22 Juni 1946 na kusainiwa na wawakilishi wa nchi 61 duniani, 'afya ni hali ya mtu kuwa vizuri kimwili, kiakili na kijamii na sio tu kutokuwa na ugonjwa au udhaifu.' Ufafanuzi huo ulianza kutumika Aprili mwaka 1948 na hadi hii leo maana hiyo ya afya haijabadika.
Ufafanuzi huo unamaanisha kwamba, tunaposema
mtu ana afya sio tu tunakusudia kuwa mwili wake hauna maradhi, upungufu
au udhaifu bali pia mtu huyo anatakiwa asiwe na matatizo ya kimwili,
kiakili na hata kijamii. Kwa mujibu wa tafisri hiyo pana ya neno 'afya'
tunaona kuwa watu wengi wanaamini kuwa afya imeganyika katika makundi
mawili muhimu ambayo ni afya ya kimwili na afya ya kiakili.
Afya ya
mwili kwa binaadamu ina maana, kuwa na mwili wenye afya usiokuwa na
maradhi, afya ambayo kwa kawaida hutokana na kuupa mwili mazoezi ya mara
kwa mara, lishe bora na mapumziko ya kutosha. Katika nchi au maeneo
ambayo watu wanapata lishe bora, huduma nzuri za afya na kuishi katika
hali ya kimaisha inayoambatana na viwango vinavyotakiwa, kwa kawaida
vimo na uzito wao huongezeka. Ukweli ni kuwa, ukiwauliza watu wengi afya
ni nini, watasema kwamba inahusiana na mwili kuwa salama bila ya
kuathirika na ugonjwa.
Lakini tukienda ndani zaidi, kitika afya ya mwili
inaamanisha ustawi wa mwili hali ambayo mtu anaipata kwa kutekeleza
vipengee vyote vinavyohusiana na afya katika maisha yake. Uzima wa mwili
unaakisi kufanya kazi vizuri moyo na mfumo wa kupumua, uwezo wa misuli,
viungo pamoja na mwili kuweza kukubali mabadiliko tofauti na muundo wa
mwili kwa ujumla. Masuala mengine ni pamoja na lishe bora, uzito wa
mwili, kutokuwepo uraibu wa madawa ya kulevya, pombe, mahusiano salama
ya kimwili, usafi kwa ujumla na pia kulala na kuamka kwa wakati
unaotakiwa.
Afya ya akili au uzima wa kiakili ni utambuzi wa mtu na uzima wake kisaikolojia. Mtu ambaye ana afya nzuri ya kiakili hana matatizo ya kiakili au kichaa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, 'afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahamili mfadhaiko (stress) unaotakana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha. Aweze kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.'
Ni rahisi watu kuelezea maana ya ugonjwa wa akili kuliko afya ya akili. Watu wengi wanakubali kwamba afya ya akili ni kutokuwepo ugonjwa wa akili lakini maana hiyo haitoshi. Hii ni kwa sababu kama tutachagua watu 100 ambao hawana kichaa au ugonjwa wa akili unaoweza kutambuliwa na daktari wa akili, lakini miongoni mwao tunaweza kuona kwamba afya ya baadhi yao kiakili imeimarika kuliko wengine.Tunaweza kusema kuwa, afya ya akili inajumuisha masuala kadhaa kama vile uwezo wa kuishi kwa furaha, uwezo wa kuvumilia shida na kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupatwa na matitizo, uwezo wa kuwa na uwiano katika maisha, uwezo wa kubadilika kwa urahisi na kuzoea mazingira mapya, kujihisi salama na kujitambua.
Majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa malaria yameonyesha mafanikio na hivyo kuleta matumaini kuwa huenda gonjwa hilo sugu linalohatarisha maisha ya mamilioni ya watoto barani Afrika likapatiwa chanjo kwa mara ya kwanza duniani. Taarifa kuhusu awamu za mwisho za majaribio ya chanjo hiyo inayotengenezwa na shirika la GlaxoSmithKline zilitangaza Jumanne ya wiki hii na kuonyesha kwamba ina uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya malaria kwa watoto wenye umri wa miezi mitano hadi 17. Andrew Witty Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo la kutengeza dawa la Uingereza ambalo limetengeneza chanjo hiyo amesema kwamba, mafanikio hayo yanaonyesha kuwa hivi karibuni dunia kwa mara ya kwanza itaweza kupata chanjo ya ugonjwa wa Malaria.

Hata hivyo sambamba na kusifu mafanikio hayo Bw.
Witty amesisitiza kwamba wanasayansi wanaoshulighulia ugonjwa huo na
wataalamu wa masuala ya afya ulimwenguni kote bado wanasisitiza kwamba
chanjo hiyo inayojulikana kana RTS,S au Mosquirix bado sio njia ya
haraka ya kutokomeza malaria. Licha ya hayo inaelezwa kuwa chanjo hiyo
ya aina ya sindano haina athari sana katika kuzuia ugonjwa wa malaria
ikilinganishwa na chanjo nyingine kama vile za ugonjwa wa polio na ndui.
Gonjwa la malaria bado ni janga kubwa kwa nchi nyingi duniani hasa za
Afrika zilizo chini ya Jangwa la Sahara na kila mwaka hupelekea vifo vya
watu wengi kwenye nchi hizo hasa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano. Chanjo sio changamoto pekee inayowakabili wataalamu wa masuala
ya afya na tiba duniani katika kupambana na malaria bali tiba ya ugonjwa
huo pia imekuwa ikibadilika mara kwa mara kutokana na vidudu vya
ugonjwa huo kujibadili na kuzishinda nguvu dawa zinazotengeneza za
kutibu ugonjwa huo.
Kwa ajili hiyo madaktari na wataalamu wamekuwa
wakishauri kutumiwa zaidi tiba ya dawa mseto katika kutibu malaria
kuliko dawa moja pekee. Njia nyingine za kujilinda na malaria ni pamoja
na kutumia chandarua, kupiga dawa za kuua mbu na kuyaweka mazingira
tuishiyo katika hali ya usafi bila kuwepo vindimbwi vya maji na
kuzungukwa na vichaka suala ambalo husababisha mbu wazaane.
Ingawa
habari hii ni mafanikio makubwa yanayopaswa kupigiwa makofi na wadau
wote wa masuala ya afya na tiba lakini, shaka yangu mie ni kuwa, hata
kama chanjo hiyo ikianza kufanya kazi kesho lakini je, watoto wote wa
bara Afrika wataweza kupatiwa chanjo hiyo na kuepusha na vifo vya holela
vinavyosababishwa na malaria? Au isije ikawa hadithi zile zile za
chanjo ya polio na ndui ambazo zimekuwepo kwa miongo mingi lakini mpaka
leo bado kuna watoto wa Kiafrika wasiopatiwa chanjo hizo kutokana na
sababu mbalimbali.
Katika hali ambayo muda mrefu imekuwa ikifahamika kwamba dawa za folic acid zinazotakiwa kuliwa na mama wajawazito zina faida kemkem kwa watoto wanozaliwa, wataalamu hivi karibuni wameendelea kufahamu umuhimu wake zaidi. Siku zote kina mama wajawazito wamekuwa wakishauriwa kula folic acid miezi mitatu kabla ya kushika mimba, na pia kwa miezi kadhaa wakati wa ujauzito.

Utafiti wa
hivi karibuni umeonyesha kwamba watoto ambao mama zao walikula folic
acid kabla na wakati wa ujauzito kwa kiasi kikubwa huwa hawachelewi
kuzungumza. Uchunguzi huo uliofanywa huko Norway kwa kuwashirikisha
wanawake 40,000 umebainisha kwamba wale ambao hawakula folic acid kabla
na wakati walipokuwa na mimba wana uwezekano mara dufu wa kuzaa watoto
wenye matatizo ya kuchelewa kuongea kuliko waliokula.
Kwa mujibu wa
utafiti huo uliochapisha kwenye Jarida la Marekani la Taasisis ya Tiba
(JAMA) kula folic acidi wiki 4 kabla ya ujauzito na kuendelea hadi wiki 8
baada ya kutungwa mimba husaidia kupunguza hatari ya watoto kushindwa
kuongea hata wanapofikia miaka mitatu. Ingawa wataalamu wamekiri hawajui
ni namna gani folic acid inazuia watoto kuchelewa kuongea lakini
wanasema, kuna uwezekano dawa hizo zikawa zinataathira katika mfumo wa
neva na kuzuia tatizo hilo lisitokee.
Folic acid ni miongoni mwa
tembe zinazohusiwa sana mama wajawazito kula, kwani inajulikana kuwa
zinazuia watoto wachanga kuzaliwa wakiwa na ugonjwa unaoitwa 'neural
tube defects' ambao ni matatizo katika sehemu ya chini ya ute wa mgongo
ambapo mtoto mchanga huzaliwa huku ubongo wake ukiwa haukukua kabisa.
Lakini ingawa hayo yote yanajuliakana shaka yangu ni kuwa je, mama
wajawazito katika nchi zetu wanajua hilo au je, wanaelimusha juu ya
umuhimu wa kula folic acid?
Nadhani ni jukumu langu mie na wewe
kuielimisha jamii.
0 comments:
Post a Comment