UKIMWI UNAZIDI KUONGEZEKA UMRI NA UPANA WAKE...... SOMA HISTORY YA UKIMWI HAPA
- Tarehe 5/6/1981 Dkt. Michael Gottlieb wa Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA)
alichapisha makala ya kihistoria ambayo yalielezea kuhusu ugonjwa wa
kushangaza ambao mpaka wakati huo ulikuwa umewakumba wanaume watano
mashoga.
- Katika
makala yake ya kihistoria, Dr. Gottlieb alibainisha kwamba wagonjwa
wote watano walikuwa wanasumbuliwa na kifua kikuu, pamoja na magonjwa
mengine nyemelezi. Ugonjwa huu baadaye ulikuja kugundulika kuwa ndiyo UKIMWI!

- Jambo
la kusikitisha ni kwamba: Kwa vile ugonjwa huu mpya ulikuwa unawaathiri
zaidi mashoga -watu ambao walikuwa hawatakiwi katika jamii hasa kwa
maoni ya wahafidhina, serikali ya Marekani haikuona haja ya kuufanyia
uchunguzi mapema na ilijikongoja sana katika juhudi zake za kuweza
kuutambua ugonjwa huu kama janga la kijamii. Mpaka wacheza sinema wa
Holywood ambao hawakuwa mashoga walipoanza kuteketea ndipo hatimaye
raisi wa Marekani wa wakati ule (Ronald Reagan)
aliweza kubadilisha mtazamo na kuutambua ugonjwa huu kuwa janga la
kijamii. Alikuwa amechelewa sana na ugonjwa huu tayari ulikuwa
umeshajitandaza...
- Baadaye iligundulika kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wagonjwa wa Hemophilia
– wagonjwa ambao wanahitaji kuongezewa damu ili kupata protini muhimu
inayosaidia damu kuganda walikuwa wameambukizwa UKIMWI. Cha kushangaza
ni kwamba, hata baada ya ukweli huu kueleweka, makampuni ya madawa ya
Marekani yaliendelea kuuza protini hii gandishi iliyokuwa imeambukizwa
katika nchi nyingine duniani. Kumbe kwa kufanya hivyo UKIMWI ukapata
nafasi ya kujitandaza zaidi ulimwenguni kwa haraka zaidi. Mpaka leo kuna
watu ambao wanaamini kwamba jambo hili lilifanyika kwa makusudi ili
kujaribu kusaidia kupunguza idadi ya watu duniani na kwamba nchi nyingi
zilizolengwa katika "kampeni" hii zilikuwa ni kutoka Afrika na nchi
zingine masikini duniani! Mpaka leo inaaminika kwamba UKIMWI umeshaua
kati ya watu milioni 28-35 na watu zaidi ya milioni 75 tayari
wameshaambukizwa !
- Nilikuwa Mwanafunzi mdogo
UKIMWI ulipoingia Bukoba. Wenyeji waliupachika jina la Juliana – jina la
mashati fulani yaliyokuwa yanatoka Uganda. Kwa tuliokuwa wote Shule ya
Sekondari ya Kahororo enzi zile nadhani watawakumbuka walimu na
wanafunzi wenzetu wapendwa tuliowapoteza kutokana na ugonjwa huu hatari
usiokuwa na tiba. Jamani, mnamkumbuka Mwalimu wetu wa Kemia Justin
Kaijage? Vipi kuhusu Mwanafunzi mwenzetu William Manhyakenda? Walimu
wetu wa Fizikia na Hesabu Mushaija na Mkewe? Vipi kuhusu Mwalimu wetu
mpendwa wa Bayolojia Ntamakurilo? Mhasibu Gama, Wapishi wetu wapendwa na
baadaye Mkuu wetu wa shule Ishengoma?
- Kama vile kitambulishi cha
ushoga kilichoambatishwa na ugonjwa huu kule Marekani, tulishuhudia
unyanyapaa mkubwa kwa wagonjwa wa UKIMWI: Ulikuwa ni ugonjwa wa kuonewa
aibu sana. Hili lilikuwa ni kosa na nchi zilizojidamka mapema katika
kukabiliana na ugonjwa huu (mf. Uganda) zilipiga hatua kubwa katika
kukabiliana nao. Nchi zingine za Kiafrika zikaendelea na unyanyapaa na
matokeo yake tumeyaona. Ugonjwa wa UKIMWI umeibuka na kuwa janga kubwa
kabisa katika kizazi hiki !
- Baada ya miaka 30,
Leo hii karibu kila familia imeshaguswa na UKIMWI kwa namna moja ama
nyingine. Mimi binafsi nilishawapoteza kaka wawili kutokana na ugonjwa
huu hatari.
- Leo hii miaka 30 ya gonjwa hili hatari tukumbuke tu kwamba bado halina kinga wala tiba na bado linaua (pamoja na Loliondo yetu!). Uzuri sasa ni kwamba tunalifahamu gonjwa hili vizuri na tunaweza kujikinga nalo tukiamua. Wapendwa, tuchukue tahadhari !!!
0 comments:
Post a Comment