Katika
makala haya tunajaribu kuwaasa wasomaji wangeweza kufikiria tutaweka nini
kwenye katiba mpya kuhusu maswala ya afya. Mojawapo ni hili la
kuhakikisha mwanadamu aliye tumboni kwa mama na aliye nje ya tumbo la
mama yaani ameishazaliwa wanatambuliwa kuwa wote ni binadamu wanaohitaji
kulindwa afya zao na kupewa huduma za afya za kuwakinga na kuwatibu.
Kwenye katiba mpya tuseme bayana kuwa mtoto aliye tumboni mwa mama yake
ana haki ya kulindwa na kutunzwa kama mtoto ambaye ameishazaliwa; awe na
haki ya kuishi na kuwa hai kama mama yake alivyo na haki ya kuwa hai na
kuishi.
![]() |
Bunge la Tanzania
|
Tanzania
ina sheria ambayo inakataza kutoa mimba. Madhumuni ya sheria hii ni
kumlinda mtoto tumboni kwa mama na vile vile inalinda afya ya mama. Sasa
mbona sheria haifuatwi kwa kumaanisha hatujasikia msichana au mama
mmoja aliyetoa mimba akapewa adhabu? Mbona hatujasikia hata daktari mmoja au mtu yeyote aliyesaidia katika kutoa mimba amepewa adhabu? Sheria
inasema anayesaidia kutoa mimba afungwe miaka kumi na mama au msichana
anayetoa mimba afungwe miaka mitano lakini hatujasikia msichana, mama,
daktari au watoa mimba wengine wamefungwa. Basi hii sheria haina maana?
![]() |
Mwanadamu wa wiki 5
|
Lakini pamoja na mapungufu haya siyo
kwamba sheria hii haina maana....
Sivyo! Kule kutofuatwa, kule kuwa hatuoni yeyote akihukumiwa vifungo vilivyotajwa na sheria vya miaka 14, 7 na 3 siyo kwamba sheria haina maana. Sheria ipo; inatukumbusha kuwa nchi yetu inaamini kuwa kila mtu hata kiumbe kilicho tumboni kwa mama kina haki ya kuishi kama ilivyo kwenye katiba ya nchi. Inaonyesha tunaamini kuweko kwa njia ya kuwasaidia walio wanyofu wasionewe na kuuawa. Kama haifuatwi basi ni kutafuta njia ya kuhimiza ifuatwe na sio kusema kuwa haina maana, haina faida.
Sivyo! Kule kutofuatwa, kule kuwa hatuoni yeyote akihukumiwa vifungo vilivyotajwa na sheria vya miaka 14, 7 na 3 siyo kwamba sheria haina maana. Sheria ipo; inatukumbusha kuwa nchi yetu inaamini kuwa kila mtu hata kiumbe kilicho tumboni kwa mama kina haki ya kuishi kama ilivyo kwenye katiba ya nchi. Inaonyesha tunaamini kuweko kwa njia ya kuwasaidia walio wanyofu wasionewe na kuuawa. Kama haifuatwi basi ni kutafuta njia ya kuhimiza ifuatwe na sio kusema kuwa haina maana, haina faida.
Inawezekana ikatokea baadaye kikundi au vikundi vikataka sheria hii ibadilishwe na eti turuhusu utoaji mimba. Ningetaka katika makala haya kuongelea misingi fulani ya kuruhusu au kutoruhusu kutoa mimba.
Jambo
la kwanza la maana ni kujua historia ya sheria za kutoa mimba
ulimwenguni na hapa kwetu Tanzania. Sheria za kutoa mimba na utekelezaji
wake zimekuwa zikibadilika badilika tangu enzi za kale. Sheria nyingi
za mwanzo zimechukua kigezo cha kutoruhusu au kuruhusu kutoa mimba kuwa
ni lini mtoto tumboni kwa mama anakuwa ni mtu hivyo kwamba ukimdhuru na
kumtoa unakuwa umemdhuru na kumuua mtu.
Sheria nyingi za zamani ziliweka kigezo kuwa uhai wa mtoto unaanza anapoanza kujitupa tupa akiwa tumboni kwa mama yaani mama anapomsikia anacheza. Huu ni wakati mama anaweza kuisikia miondoko na mapigo ya mtoto akiwa tumboni mwake.
Badaye kwenye karne ya 18 na
ya 19 watu wakafikiri zaidi na kuona kuwa mtoto aliye tumboni kwa mama
ni mtu hata kabla hajaanza kupiga piga na kusukuma sukuma. Hapo basi
wakatunga sheria za kutoruhusu utoaji mimba kabisa wakati wowote.
Walijua na kuamini kuwa uhai wa mtoto unaanza mara mimba inapotungwa
yaani mbegu na yai vinapokutana.
Ilipokuja
karne ya 20 yaani karne iliyopita swali la utoaji mimba likawa siyo la
sayansi tena. Likaingiliwa na wapigania haki za wanaoonewa kwa njia moja
au nyingine na hata na watetezi wa haki za kina mama. Nchi nyingi za
magharibi zikaanza kuruhusu utoaji mimba bila hata kufikiria anayetolewa
kwenye mwili wa mama ni mwanadamu; mradi tu haki ya mama kwamba mwili
ni wake na anaweza kufanya analotaka na mwili wake. Haikuzingatiwa kuwa
kiumbe kilichopo tumboni mwa mama nacho kina haki.
Hata
hivyo wakati wa vugu vugu kubwa la kumkomboa mwanamke kutoka kwenye
uonevu; viongozi wanaharakati huko Amerika hawakukubali utoaji mimba na
walidiriki kusema, “Hata kwa sababu ipi, hata kama ni kupunguza matatizo
au kwa nia ya kumuokoa mtoto kutokana na matatizo ambayo unafikiri
atayapata baada ya kuzaliwa, mwanamke anayefanya kitendo cha kutoa mimba
hujisikia hapo hapo na baadaye dhamira yake ikimsuta vibaya sana kwa
kujua na kujisikia kuwa kitendo alichofanya ni kibaya sana. Kitendo
hiki kitamwelemea kwenye dhamira yake maisha yake yote. Yule mtu
aliyemfanya akaamua hivyo na aliyemsaidia kuitoa hiyo mimba naye hupata
mateso ya mara 3 ya huyu mama”
Huko
Ulaya karne ya 18 utoaji mimba uliruhusiwa kabla ya mtoto tumboni
kuanza kujitupa tupa yaani kabla ya mama kumsikia anacheza cheza.
Baadaye kwenye karne ya 19 utoaji mimba ukakatazwa kabisa.
Tena
baadaye, karne ya 20 mataifa ya magharibi yakaruhusu utoaji mimba.
Katika karne mbili za 18 na 19 kuruhusu au kutoruhusu utoaji mimba
kulitegemea na kuelewa kwa wanadamu kuwa kiumbe kilichopo tumboni,
ubinadamu wake unaanza lini.
Karne
ya 18 ilikuwa imeeleweka kuwa mimba ikiishatungwa mimba hiyo inakuwa
mwanadamu wakati wa mtoto anapoanza kujitikisatikisa tumboni. Kwa hiyo
walifikiri utoaji mimba kabla mtoto tumboni hajaanza kujitupa tupa;
kabla mama hajamsikia akicheza cheza ilikuwa ni sawa. Karne
ya 19, sayansi ikawa imeendelea zaidi na kuonyesha kuwa mimba
ikiishatungwa hapo hapo anayetokea ni mwanadamu anayeanza safari yake ya
kukua. Hapo ndipo ikabidi sheria ibadilike iseme hakuna ruksa kutoa
mimba tena kwa sababu ukitoa mimba unaua binadamu. Sheria zilitungwa
karne ya 19 zikikataza kutoa mimba kwani mimba ikishatungwa, anayetokea
ni binadamu na unapomuua kwa utoaji mimba unaua binadamu.
Wiki
ijayo tutaangalia kuwa ilipofika karne ya 20 watu wa magharibi wakarudi
nyuma tena, wakakataa kuendelea kukubali jambo la kisayansi kuwa
mwanadamu anaanza kuwa mwanadamu wakati mbegu na yai wanapokutana. Wakafuta sheria za karne ya 19 zilizokataza utoaji mimba na wakatunga sheria kuruhusu utoaji mimba.
Tuandikie
kama una maoni na maswali juu ya utoaji mimba; ni sawa au siyo sawa.
Tuandikie uzoefu wako kama umeishatoa mimba au kama unamjua ndugu,
rafiki nakadhalika aliyetoa mimba na tuambie yaliyomkuta. Barua zote ni
siri tuma kupitia kiboksi cha maoni kilichopo pembeni kulia au tuma kupitia e-mail; fyatele@gmail.com
Washkaji wakijadiliana;
Mshkaji 1 :Naambiwa kubadilisha sheria ya kutoa mimba huko Ulaya kulihusu vile vile haya mambo wanayozungumzia Wazungu.
Mshkaji 2 : Mambo gani?
Mshkaji 1:
Naona haya kuyasema kwani kwetu siyo tu hairuhusiwi kuyafanya bali hata
kuyasema. Ni haya mambo ya wenzetu huko magharibi ya wanaume eti kulala
na wanaume. Huko nyuma walikuwa na sheria kuwa ukihisiwa tu na siyo
wala wakukamate kuwa wewe mwanamme unalala na wanaume wanakunyonga au
wanakuwekea kuni na manyasi na kukuchoma moto hapo hapo walipokukamatia.
Baadaye wakabadilisha wakasema ni sawa tu wanaume walale na wanaume.
Mshikaji 2:
Mamaaaa! Ni hivyo hivyo kwa sheria ya kutoa mimba kuwa huko mwanzoni
ukitoa mimba wanakunyonga au kukufunga maisha na sasa ukitoa mimba haina
noma!
Mshkaji 1: Kweli kumbe hizi siyo tu nchi zilizoendelea bali ni nchi zilizogeuka.
0 comments:
Post a Comment