kwa kifupi tu ni kwamba ili mtu awe na uzazi salama anapaswa kujua yale
mambo yanayoweza kuathiri mfumo wake wa uzazi ili kuweza kujiepusha
nayo.
Mfumo wa uzazi unaweza kuathiria na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na
magonjwa ya ngono ambayo hushambulia mfumo huo, leo tutajadili baadhi
ya magonjwa hayo ambapo tutapata kujua majina yao, jinsi
yanavyoambukizwa, dalili na kinga au tiba zao ijapokuwa kipengele cha
tiba sitakiongelea kwa undani.
1. KISONONO:
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi na hushambulia zaidi sehemu za siri za jinsia zote.
Dalili;
Dalili kuu za ugonjwa huu ni mgonjwa kutokwa na usaa kwenye sehemu za
siri na mgonjwa kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo,
na ukikaa kwa muda mrefu bila kutibiwa huenea zaidi kwenye viungo
vingine vya uzazi.
Kuzuia/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni kuacha kujamiiana au kutumia kondom kwa kila tendo la ngono.
na kwa wale ambao tayari wanamaambukizi wanashauriwa kutibiwa wote hospitalini na kuacha kufanya ngono hadi wapone.....
2. KASWENDE:
Huu ni ugonjwa wa ngono unaosababishwa na bakteria.
Dalili;
Mgonjwa wa Kaswende hupata mwasho mkali sehemu za siri na kupata
vijeraha vidogo vidogo sehemu hizo na akikaa sana na ugonjwa huo bila
kutibiwa huweza kuathirika sehemu zingine za mwili kama vile, Moyo,
ubongo na hatimaye kusababisha kifo.
Kinga/ Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni; kuacha kujamiiana na ukishindwa kuacha kabisa basi fanya ngono iliyo salama(yaani utumie Condom)
Ugonjwa huu hutibiwa Hospitalini na inashauriwa wenza wenye ugonjwa huu watibiwe kwa pamoja.
Wakati wa matibabu maswala ya kujamiiana yawekwe kando hadi matibabu yakamilike kwani yanaweza yakaongeza maambukizi mapya.
3. KLAMEDIA:
Huu ni mojawapo ya magonjwa ya ngono ambao haujafahamika unaambukizwa na wadudu wa aina gani.
Dalili;
Mgonjwa wa klamedia hutokwa na uchafu katika sehemu zake za siri na
kupata maumivu makali wakati wa haja ndogo na wakati wa kujamiiana.
Kinga/Tiba;
Kinga ya ugonjwa huu ni sawa na kinga ya magonjwa mengine ya zinaa, ili
usiupate ugonjwa huu unashauriwa kuacha kabisa kufanya ngono au kutumia
condom kwa kila tendo la ndoa.
Hugonjwa huu pia hutibiwa hospitalini.
4. TRIKOMONA:
Ugonjwa huu husababishwa na protozoa (trikomonasi vaginalis) ambazo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
Dalili;
Dalili za ugonjwa huu hutofautiana kwa kila jinsia.
WANAWAKE: Wanawake wenye ugonjwa huu hupatwa mwasho mkali katika sehemu za siri,
Hutokwa na uchafu wa rangi ya njano au kijani wenye harufu mbaya sehemu za siri.
WANAUME: Wanaume wenye ugonjwa huu hupata maumivu makali wakati wa haja ndogo.
Kinga/ Tiba;
Ugonjwa huu pia unazuilika kwa kuacha kujamiiana au kutumia condom kwa kila tendo la ngono.
Mgonjwa atatibiwa hospitalini na kupona kabisa.
5.UKIMWI:
malizia wewe maelezo yake kama kweli unakwenda na matukio ya jamii na nchi yako kwani kama ingekuwa wimbo wa dunia basi hii ndiyo ingekuwa Chorus ya wimbo wa gonjwa sugu la dunia
pia tunakaribisha maoni juu ya Afya ya uzazi, kwa lengo la kusaidia jamii kupata afya tele kupitia kiboksi cha kuandika na kutuma maoni pembeni kulia au e-mail afyatele@gmail.com au andika hapa chini.
(kwa utakayetuma kwa e-mail au kiboksi cha maoni itakuwa siri).
Friday, 11 July 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment