
Ingawa
katika mahusiano wanawake na wanaume hukasirika katika kiwango cha kufanana,
katika uzito wa kukasirika huko na urefu au ufupi wa hasira hizo, tafiti
zinaonyesha kwamba wanaume huhusisha fujo, magomvi, kupigana na hata uharibifu
“violence” wanapokuwa na hasira
kuliko walivyo wanawake. (Ingawa wako wanawake wachache wenye fujo pia). Sasa
labda hii itakusaidia kujua kwanini wanawake hukasirishwa sana tu lakini ni
rahisi mkaongea na akapoa wakati mwanaume anapokasirishwa muda mfupi tu, tayari
anakuwa kashanyanyua mkono na mtu kashachapwa vibao, ngumi, kurushiwa vitu, na
akikusamehe sana basi ndiyo utaishia kutukanwa kila aina ya tusi na maneno
mazito kama vile yeye kamwe hajawahi kumuudhi mtu. Ni vema wewe mwanaume ukajua kuwa sio wote wenye
uwezo wa kukuvumilia hiyo tabia yako, maumivu hayazoeleki hata sikumoja,
utakuja kugundua kuwa mpenzi wako alikuwa anaumia mwili na moyo pale
atakapoacha kukupenda, kukuheshimu, kukujali na labda hata kukukimbia – Kwa hisani ya Chris Mauki.
0 comments:
Post a Comment