Vipimo
Viazi 2
Karoti 2
Koliflawa (cauliflower) ½
Brokoli 3 misongo (bunch)
Pilipili mboga ya kijani 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Pilipili manga iliyosagwa 1 kijiko cha chai
*Kidonge cha supu (stock) 1
Chumvi kiasi
Mafuta ya zaytuni (olive oil) 3 vijiko vya supu
Maji ½ kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi katakata vipande vya mchemraba (cubes)
- Katakata karoti vipande vya duara
- Katakata pilipili mboga vipande vya kiasi kiasi
- Chambua koliflawa na brokoli
- Changanya vitu vyote kwenye sufuria pamoja funika kisha weka katika jiko kwa moto mdogo mdogo.
- Ikishawiva kidogo tu ipua mimina kwenye bakuli tayari kuliwa na mkate au wali.
0 comments:
Post a Comment