Wanasayansi
wanasema kuwa wamefanya ugunduzi mkubwa katika jitihada za kutibu
ugonjwa wa Ukimwi kwa kulazimisha virusi kuondoka katika maficho yao
mwilini.
Virusi vya
HIV huganda na kujificha katika DNA ya mgonjwa na kuishi humo kwa miaka
mingi bila ya kufanya chochote, hali ambao inatatiza juhudi za kupata
tiba.
Awamu ya
kwanza ya utafiti huo uliofanyiwa wagonjwa sita, ilionyesha kuwa
matibabu ya chemotherapy ambayo hupewa wagonjwa wa Saratani, kwa kiwango
kidogo yanaweza kuamusha virusi hivyo kutoka katika maficho yao.
Wataalamu wanasema matokeo haya ni ishara nzuri , lakini huenda isiwezekane kwa matibabau hayo kuangamiza virusi vya HIV kabisa.
Dawa za
kupunguza makali ya HIV, zinaweza kupunguza idadi ya virusi kwenye damu ,
maana kwamba waathiriwa wa HIV wanaweza kuwa na maisha ya kawaida tu
licha ya kuwa na virusi mwilini.
Lakini kuna
tatizo moja hapa. Virusi vya HIV pia vinaweza kugandisa DNA yake kwenye
DNA ya binadamu, na hapo inakuwa changamoto kwa matibabu kwani dawa
haziwezi kivifikia.
Wakati mgonjwa anapoacha kutumia dawa zake, virusi hivyo huamka upya na kuanza kushambulia mwili.
Utafiti sasa unalenga kuangalia mbinu za kuondoa virusi hivyo kutoka katika maficho yao na kuviua.
Kikundi cha
madaktari kutoka chuo kikuu cha Aarhaus nchini Demark, walijaribu
kutumia dawa inayotumiwa katika matibabu ya Chemotherapy, Romidepsin,
ambayo hutumiwa kwa wagonjwa wa Saratani.
Wagonjwa sita ambao waliokuwa na kiwango kidogo sana cha virusi mwilini, walihusishwa katika utafiti huo
Wote walipatiwa dawa ya Romidepsin mara moja kwa wiki katika kipindi cha wiki tatu.
Katika wagonjwa watano, kiwango cha virusi mwilini kilipanda.Ishara kuwa virusi hivyo vilikuwa vinatoka katika maficho yao.
Mmoja wa
madaktari waliohusika na utafiti huo,Dr Ole Sogaard, alisema kila hatua
ya utafiti wa kutafuta tiba ya HIV ni muhimu kwake na humpa raha.
Alisema licha ya ugunduzi wao, baadhi ya watu wana shaka na matibabu hayo wakisema haitoshi kuua virusi.
"tumeonyesha
tunaweza kuondoa virusi kutoka katika maficho yao , hatua itakayofuata
ni namna ya kuua virusi hivyo, '' alisema daktari Ole Sogaard "hatua itakayofuata ni kuchanganya dawa ya Romidepsin ili kuimarisha kinga ya mwili, na hii kwetu sisi itakuwa chanjo ya HIV. ''
athari zinazotokana na matibabu haya ya Chemotherapy,ni pamoja na uchomu mwilini.
Moja ya
changamoto ya matibabu haya ni kwamba madaktari hawawezi kusema kiwango
cha virusi vya HIV kinachotolewa kutoka katika maficho yao.
Habari na BBC Swahili
Video na Temple University School of Medicine research team's
0 comments:
Post a Comment