-

-

-

-

-

Habari Mpya

Sunday, 3 August 2014

SALADI YA TAMBI NA JIBINI (cheese)

Tambi nimoja ya vyakula visivyokua na asili ya Africa ,asili yake ni Italia.Nichakula kikuu cha watu wa italia kama ilivyo ugali kwa watanzania.
Miaka hii yakaribuni  tambi  zimekua chakula cha kawaida kwa waafrika wengi.
Saladi ya Tambi na Jibini
Saladi ya Tambi na Jibini
Kuna tambi za aina mbalimbali ,zenye ladha na maumbo tofauti.Upishi wake nao  watofauti kutokana na aina ya tambi.Unaweza andaa tambi kama chakula kikuu ,kama salad ,au kama kitafunwa,hutokana tu na aina ya tambi utakayochagua na jinsi utakavyoiandaa.
Mahitaji
  • Tambi paketi 1 -zenye umbo la spiringi
  • Jibini kavu kikombe 1:Sugua kwa sugulio la karoti (shred)
  • pilipili hoho zakijani 3 kubwa-kata vipande vinene kwa urefu
  • Pilipili hoho nyekundu Moj:kata vipande vinene kwa urefu kisha gawanya kila kipande mara mbili
  • Giligiliani kavu kijiko 1 cha chakula :saga mbegu kavu za giligiliani
Njia
1.chemsha maji  mengi adi yatokote (lita mbili).ongeza tambi,acha zichemke adi ziiive .
  • Usiache ziwe rojo hazitapendeza
2.katika kikaango au sufuria zito weka pilipili hoho za rangi zote,kisha weka jikoni katika moto mdogo,geuza kila mara adi zote zipate joto nakuanza kusinyaa kisha weka pembeni
  •   Usiongeze kitu chochote kwenye pilipili hoho
3.Tambi zikiiva chuja maji yote kisha weka tambi kwenye bakuli la chuma au sufuria pana
  •     Chuja maji mara tu tambi zikiiva,usiache zipoe wala kupoteza joto
4.katika Bakuli la tambi ongeza pilipili hoho.nyunyuzia chumvi na unga wa giligiliani kisha nyunyuzia jibini na changanya vizuri.
Saladi tayari kwa kula.Unaweza kula salad hii na vyakula vingine au ukaifanya sehem kuu ya mlo wako.Ni vyema kujua kwamba saladi si lazima ziwe mboga za majani peke yake,yaweza kua mchanganyiko wa mboga za majani na vyakula vingine kama ilivyo salad hii.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SALADI YA TAMBI NA JIBINI (cheese) Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top