Mada hii ina lengo la kuzungumzia tatizo la kuwa na hofu au wasiwasi uliopita kiasi au kwa kitaalamu Generalized anxiety disorder (GAD). Kwa ajili ya kutofautisha kati ya hofu iliyopitiliza na hofu ya kawaida ambayo yaweza kumkumba mwanadamu yeyote, wakati fulani fulani mwandishi atatumia maneno anxiety au GAD katika kuwasilisha ujumbe wake.
Hofu iliyopitiliza au au anxiety au GAD huambatana na hali ya kuwa na wasiwasi kupita kiasi juu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio yake bila hata muhusika kuwa na sababu maalum ya kuwa na hofu hiyo. Kwa maneno mengine ni kuwa, watu wenye anxiety hujihisi hofu kubwa bila ya kuwa na sababu yeyote ya msingi ya kuwafanya wawe hivyo. Mara nyingi watu wenye tatizo hili huwa na tabia ya kuhisi kwamba janga kubwa litawatokea karibuni au maafa yatamkumba katika maisha yake na daima hawaachi kuwa na hofu isiyo na sababu juu ya familia zao, pesa, afya, ajira, masomo au hata biashara zao.
Maisha yao ya kila siku huwa na mchanganyiko wa hofu, wasiwasi na huzuni, kiasi kwamba hatimaye hofu hutawala mawazo ya muhusika kiasi cha kuingilia utendaji wake wa kila siku ikiwemo kazi, masomo, shughuli zake za kijamii, na hata mahusiano na mwenza wake wa ndoa.
Dalili za hofu iliyopitiliza (anxiety) ni nini?
Kama tulivyoona hapo juu kwenye utangulizi, hofu isiyo na kikomo huathiri zaidi uwezo wa mtu katika kufikiri, ingawa baadaye humletea matatizo ya kiafya katika mwili. Hali hii inaweza kuambatana na dalili mbalimbali, siyo tu zile zinazohusu uwezo wa kufikiri na akili bali hata zinazohusiana na utendaji kazi wa mwili.
Baadhi ya dalili hizo ni:
- Kuwa na hisia ya kuwepo kwa janga, kwamba kitu kibaya kitatokea muda wowote, na kwamba hatari kubwa inamnyemelea
- Hali ya hofu kuu
- Hali ya kujihisi kutaka kukimbia, kuondoka mbali na hatari hiyo
- Rangi ya ngozi kuwa ‘nyeupe’ kama mtu aliyeishiwa damu
- Kujihisi ngozi kuwaka moto
- Hali ya koo kubana, kujihisi kama koo limefunga, au umekabwa na kitu kooni
- Hali ya kuchanganyikiwa
- Kujihisi kutengwa na ulimwengu, kupoteza hisia, kupoteza kujitambua nafsi yako mwenyewe
- Kujihisi kama mtu anayeota
- Kizunguzungu, kuhisi kichwa kuwa chepesi, kupepesuka unapotembea
- Kuwa na mvurugano wa hisia
- Hofu ya kurukwa akili
- Hofu ya kupoteza uwezo wa kujithibiti mwenyewe
- Kujihisi kama vile kuna kitu kinachobana kichwani (kama uliyezungushiwa kamba au rubber-band)
- Kujihisi baridi sana au joto sana (ingawa hali ya hewa yaweza kuwa kinyume)
- Kushindwa kujituliza
- Kujihisi kitu kinabana tumboni
- kichefuchefu
- kujihisi ganzi au hali ya kuchomachoma sehemu fulani fulani za mwili
- kuwa na hisia za kupanic
- kuhisi kuziba masikio
- moyo kudunda sana
- Moyo kwenda kasi isivyo kawaida
- Maumivu makali kifuani, shingoni, kwenye bega, kichwani au usoni
- Hali ya kuhisi kukosa hewa au kupumua kwa shida
- Kutokwa na jasho
- Kubanwa na kifua
- Kutetemeka (kunaweza kuonekana waziwazi au kutetemeka kwa ndani bila mtu mwingine kutambua)
- Kuchafuka kwa tumbo
- Kujihisi haja ndogo au kubwa mara kwa mara
- Kutapika
- Uchovu wa mara kwa mara
- Shida ya kupata usingizi au kulala usingizi wa mang’amung’amu
Hofu iliyopitiliza (GAD) husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha matatizo ya kuwa na hofu kupita kiasi hakifahamiki. Hata hivyo kuna baadhi ya vitu ambavyo vimegundulika kuwa vinachangia sana kuwepo kwa tatizo hili miongoni mwa watu.
Vitu/mambo hayo ni pamoja na:
• Nasaba (genetics): baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa nasaba ina nafasi kubwa ya kumfanya mtu wa familia yenye matatizo ya hofu iliyopitiliza naye kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata haya. Hii inaamnisha kwamba, hofu iliyopitiliza inaweza kurithiwa miongoni mwa wanafamilia.
• Mfumo wa kemikali za ubongo: Kuwepo kwa hofu iliyopitiliza kumehusishwa na kuwepo kwa kiwango kisicho sahihi cha baadhi ya kemikali zinazosaidia kusafirisha taarifa katika ubongo yaani neurotransmitters. Kazi ya kemikali hizi ni kupitisha taarifa na ujumbe mbalimbali kutoka seli moja ya neva mpaka seli nyingine. Iwapo kemikali hizi zitakuwa katika kiwango kisicho sahihi (ama kupungua au kuongezeka) taarifa hazitaweza kusafirishwa kati ya seli za neva na hatimaye hazitaweza kuufikia ubongo inavyotakiwa. Hali hii inaweza kusababisha mabadiliko katika utendaji kazi wa ubongo na hatimaye kusababisha mtu kupatwa na hofu iliyopitiliza.
• Sababu za kimazingira: matukio kama vile ajali, kuumia au matukio yenye msongo mkubwa kama vile kunyanyaswa kwa namna yeyote ile, kufiwa na mtu unayempenda, talaka, kubadilisha kazi au kuachishwa/kufukuzwa kazi, kubadilisha shule au kufukuzwa/kuacha shule nayo pia yanaweza kusababisha kuwa na hali ya hofu iliyopitiliza. Hofu (GAD) pia huwa mbaya zaidi kipindi ambapo muhusika huwa katika hali ya msongo mkubwa wa kimaisha (stress). Aidha matumizi ya vitu vyenye kulevya kama pombe (alcohol), sigara (nicotine) au hata kahawa nayo pia yanaweza kuongeza ukubwa wa tatizo hili. Kadhalika, watu waliokuwa watumiaji wakubwa wa vitu hivyo kisha wakaacha ghafla, nao wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na tatizo hili.
Ukubwa wa tatizo
Bahati mbaya, takwimu za ukubwa wa tatizo nchini Tanzania hazikuweza kupatikana. Hata hivyo, inakadiriwa kuwa takribani watu wazima milioni 4 mpaka 5 huko nchini Marekani hukumbwa na tatizo hili kila mwaka.
Kwa kawaida, wanawake huathiriwa zaidi kuliko wanaume. Aidha hofu iliyopitiliza mara nyingi huanza kipindi cha utoto au utoto kabla ya ujana ingawa pia inaweza kutokea wakati wa utu uzima.
Vipimo na uchunguzi
Iwapo mgonjwa ana dalili za hofu iliyopitiliza, kwanza daktari atataka kufahamu historia yake kwa kumuuliza maswali juu ya maisha yake na dalili zinazomsumbua kabla ya kumfanyia uchunguzi wa mwili mzima ili kufahamu kama hana tatizo jingine la mwili linaweza kumletea dalili kama hizo.
Kuweza kutambua kama mgonjwa ana tatizo hili, daktari atatilia mkazo kwenye ukubwa wa tatizo lenyewe, muda tangu dalili zilipoanza kujitokeza, na iwapo tatizo hili linamfanya mgonjwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Iwapo daktari ataweza kubainisha katika historia ya mgonjwa kuwa mgonjwa amekuwa akisumbuliwa na dalili hizi karibu kila siku (au muda mwingi) katika kipindi cha miezi sita, hapo tunaweza kusema kwa hakika kuwa ni kweli mgonjwa ana tatizo la hofu iliyopitiliza (GAD). Dalili hizi pia ni lazima ziingilie na kuathiri mfumo wake wa maisha ya kila siku.
Pamoja na kuwa hakuna kipimo cha kuweza kugundua ugonjwa huu, daktari pia anaweza kuagiza kufanyika kwa vipimo vingine ili kuchunguza iwapo mgonjwa ana tatizo jingine lolote la kiafya.
Matibabu
Iwapo uchunguzi utaonesha mgonjwa hana tatizo lolote la kiafya katika mwili, daktari atampeleka kwa wataalamu wa masuala ya afya ya akili kwa ajili ya matibabu zaidi. Matibabu ya tatizo hili kwa kawaida hujumuisha matumizi ya dawa pamoja na tiba isiyohitaji dawa (au tiba ya kujitambua yaani cognitive-behavioral therapy).
• Matumizi ya dawa: kwa watu ambao tatizo hili linaingiliana na maisha yao ya kila siku, matumizi ya dawa yameonekana kusaidia sana kuwafanya warejee katika hali yao ya kawaida. Dawa hizo ambazo pia huitwa tranquilizers husaidia kumtuliza mgonjwa na kumfanya ajihisi kupumzika. Dawa zinazotumika zipo katika jamii ya benzodiazepines nazo hufanya kazi ya kupunguza dalili za GAD kama vile kukaza misuli ya mwili au hali ya mgonjwa kutotulia. Baadhi ya dawa zilizo kwenye jamii hii ni kama vile diazepam (valium) na Ativan. Jamii nyingine ya dawa ni zile za kuondoa msongo wa mawazo (depression) yaani Antidepressants, kama vile Prozac, na Zoloft. Hizi nazo hutumika katika matibabu ya muda mrefu ya watu wenye hofu iliyopitiliza.
• Tiba ya kujitambua (cognitive-behavioral therapy): watu wenye matatizo ya hofu iliyopitiliza wanaweza pia kupatiwa tiba hii ambapo mgonjwa hufundishwa jinsi ya kutambua na kubadili namna anavyofikiri na tabia zinazomfanya awe na hisia za hofu. Aina hii ya tiba husaidia kuzuia kuibuka kwa mawazo ya hofu kwa vile humfanya mgonjwa kuyachunguza na kuziangalia hofu zake katika hali ya uhalisia.
Aidha mbinu mbalimbali za kuutuliza mwili (relaxation) kama vile kuvuta pumzi nyingi ndani kisha kuiachia taratibu nazo pia husaidia kuondoa kukaza kwa misuli kunakoambatana na kuwepo kwa hofu iliyopitiliza.
Pamoja na kwamba baadhi ya watu wenye tatizo hili hawawezi kutibiwa na kupona moja kwa moja kwa kuwa bado huendelea kupatwa na dalili hizi kwa kitambo fulani fulani, wengi wao hupata nafuu ya uhakika iwapo watapata tiba sahihi na wakatilia mkazo unaotakiwa kwenye tiba hiyo.
Kinga
Je kuna kinga dhidi ya tatizo hili?
Hofu iliyopitiliza haina kinga. Hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo husaidia sana kupunguza makali ya dalili za tatizo hili. Mambo hiyo ni pamoja na:
- Kuacha au kupunguza matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile kahawa, chai, cola au chokoleti.
- Kuepuka kutumia dawa zozote zenye vitu vinavyoweza kuchochea kutokea kwa hali bila kupata ushauri wa kitaalamu.
- Kujitahidi kufanya mazoezi ya mwili kila siku
- Kutafuta msaada wa ushauri nasaha pindi unapopatwa na matatizo yenye kuumiza moyo/nafsi, na
- Kujifunza kuthibiti msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi mbalimbali kama vile yoga
Dalili na Viashiria vya Upungufu wa Akili
- Kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza
- Upungufu wa kumbukumbu (deficits in memory skills)
- Matatizo katika kufahamu mambo ya kijamii
- Upungufu wa uwezo wa kutatua matatizo
- Kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe (kama kufunga vifungo vya shati nk)
- Kuendelea kuwa na akili za kitoto
- Kupungua uwezo wa kusoma
- Lack of social inhibitors
- Kushindwa kufikia vigezo vya ukuaji wa kiakili
- Kushindwa kumudu masomo shuleni
- Lack of curiosity
Utambuzi wa Upungufu wa Akili Utambuzi wa upungufu wa akili huusisha
- Historia ya mgonjwa – Kuhusu mazingira ya sehemu anayoishi, matumizi ya madawa ya aina yoyote, historia ya magonjwa ya akili, tabia ya awali na ya sasa ya mgonjwa, tiba aliyowahi kupata kuhusu ugonjwa wa akili, jinsi familia na wahudumu ya afya wanavyomchukulia kuhusu hali yake na nk.
- Vipimo vya afya
- Vipimo vya mfumo wa fahamu
- Mental status examination –Hufanywa na daktari
- Vipimo vya uchunguzi – Vipimo vya ugonjwa wa kaswende, Rubella, Toxoplasmosis, Cystomegalo virus, Herpes simplex, vipimo vya mkojo (kuangalia phenylketonuria), kipimo cha EEG kama amewahi kupata degedege, vipimo vya damu na nk.
- Vipimo vya saikolojia - The Bayley Scales of Infant Development, The Stanford-Binet Intelligence Scale, The Wechsler Intelligence Scale for Children-III, and The Wechsler Preschool and Primary Scale of Intelligence-Revised.
- IQ ya 70 au chini yake wakati mgonjwa anafanyiwa kipimo cha akili (IQ test). kwa mtoto mchanga, hupimwa uwezo wa ufanyaji kazi kwa vipimo vya kliniki (clinical judgement)
- Kutokuwa na uwezo au upungufu katika kujihudumia mahitaji yake ya kimaisha kutokana na umri wake au utamaduni wake, kuwepo kwa angalau vigezo viwili kati ya hivi basi mgonjwa ndio anatambuliwa kuwa na upungufu wa akili, vigezo hivyo ni kama vifuatavyo;
b. Kushindwa kujihudumia katika suala zima la usafi, mavazi, chakula (self care) na kushindwa
c. Kuishi nyumbani
d. Kujumuika na watu
e. Kutumia huduma za jamii
f. Kutokuwa na muelekeo (self direction)
g. Kutokuwa na akili darasani au kushindwa kumudu masomo
h. Kushindwa kufanya kazi
i. Kushindwa kustarehe (leisure)
j. Afya (health)
k. Usalama (safety)
l. Kutokea kwa tatizo hili kabla mtu kutimiza miaka 18
Tiba ya Upungufu wa Akili Tiba ya mtu mwenye upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili
a. Huduma za mtu mwenye upungufu wa akili
- Muathirika kuhudumiwa nyumbani na familia pamoja na familia kupewa elimu ya kijamii ili kuweza kumhudumia
- Muathirika kuishi katika nyumba za kijamii (foster home) au group home
- Rehabilitation centers
- Asasi za kijamii kusaidia familia ili kuweza kumudu gharama za kumhudumia ndugu au jamaa yao wenye upungufu wa akili.
- Ushauri nasaha kwa familia ili kuweza kuhimili msongo wa mawazo pamoja na tabia za mtu mwenye upungufu wa akili
- Tiba sahihi kwa matatizo ya kisaikolojia pamoja na tabia za mtu wa upungufu wa akili
- Behavioral modification (using positive and negative reinforcement principle)
- Matatizo ya kiafya kama degedege yanahitaji tiba sahihi
- Kumpima uwezo wake wa kiakili mara kwa mara ili kujua ni mahitaji gani ya shule muathirika anahitaji. Kupima mara kwa mara ni njia sahihi kwani wengi hupata nafuu au huonesha maendeleo mazuri na hivyo mahitaji kubadilika kadri muda unavyokwenda
- Shule maalum
- Tiba ya sauti au lugha (speech/language therapy) kutoka kwa madaktari bingwa wa kutibu sauti (Speech/language therapists)
- Behavioral therapy – Matibabu ya kurekebisha tabia ya muhusika
- Occupation therapy
- Huduma za kijamii kwa familia na muhusika
- Kubadilisha mfumo wa maisha (health lifestyle) kula lishe bora, kufanya mazoezi, kujihudumia, kupunguza msongo wa mawazo kwa wenye upungufu wa akili
- Ushauri nasaha mara kwa mara au kuhudhuria program maalum za ushauri nasaha na mambo ya kijamii
- Dawa za ugonjwa wowote wa akili muhusika alionao (antipsychotic medications)
- Dawa za maumivu kulingana na kiwango cha maumivu
- Mawasiliano kwa kutumia maandishi, sauti au picha na hata lugha ya vitendo kwa watu wenye upungufu wa akili ili kuleta maelewano wakati wa tiba na kumfanya muathirika kupata hamasa ya kuendelea na tiba
- Kuwafanyia uchunguzi kama wananyanyaswa kijinsia kama kubakwa nk. Watu wenye upungufu wa akili mara nyingi hubakwa na hivyo kuwafanya kuwa wakali au kuwa na hasira. Daktari anahitajika kugundua anapoona ishara hii kwa mgonjwa wakati wa kumpima.
- Kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga watu wenye upungufu wa akili
1. Kinga ya awali (Primary Prevention)
- Kuboresha huduma za afya na kijamii ili kuondoa tatizo la utapia mlo, kuongeza uhamasishaji, kuondoa tatizo la kuzaa watoto njiti, na kutoa elimu kwa kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya, unywaji pombe, magonjwa ya zinaa na nk wakati wa ujauzito
- Kuboresha huduma za afya za kina mama, tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuzuia maambukizi, ajali (trauma), madhara mbalimbali wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba, na magonjwa ambayo yanaweza kumuathiri mtoto kabla, wakati na baada ya kuzaliwa.
- Mtoto kupata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa wa polio, ugonjwa wa surua na nk.
- Kuwaelimisha kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya na umuhimu wa kuhudhuria kliniki
- Kutoa ushauri nasaha kwa wazazi ambao wanaathari za viashiria vya asili (genetic counseling to high risk group)
- Kufanya tafiti juu ya sababu au vyanzo vya upungufu wa akili pamoja na tiba yake.
- Kuwaelimisha mama wajawazito jinsi ya kujifungua salama na umuhimu wa kuwasikiliza wahudumu wa afya wakati wa kujifungua kwani mara nyingi kina mama huwakosesha watoto wao hewa na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata upungufu wa akili na ndio sababu wahudumu wa afya wanakuwa wakali sana kwa kina mama wanaofanya hivyo kuchelea mama asipate mtoto mwenye tatizo hili. Hii itasaidia kuondokana na ile dhana ya kwamba kujifungua hospitali za serikali kwa mama mjamzito ni adhabu kwani huwa wanapigwa.
- Ugunduzi wa mapema na tiba sahihi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika kama phenylketonuria, hypothyroidism nk.
- Ugunduzi wa mapema wa matatizo katika mfumo wa fahamu, mabadiliko ya tabia na hisia ili kukabiliana nayo mapema.
- Ugunduzi wa magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa kaswende, Rubella nk mapema kabisa ili muathirika apate tiba haraka
- Kufanya kipimo cha Ultrasound, CT, MRI, mapema ili kuweza kugundua kama mtoto ana kilema chochote katika maumbile, hii itasaidia kupanga na kumhudumia mapema zaidi ili kudhibiti tatizo.
- Ugunduzi wa upungufu wa akili mapema zaidi kwani kuchelewa kutambua huchelewesha tiba yake..
Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya utambuzi na kutafakari (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.
Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.
Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology) Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.
Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV) kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18. Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).
Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni nini?
Tabia za kuendana na mazingira ni jinsi mtu anavyoweza kumudu matakwa ya kujihudumia mwenyewe kila siku pasi na kumtegemea mtu yoyote kutokana na umri wake, tabaka lake, utamaduni pamoja na jamii inayomzunguka kutokana na vipengele viwili kati ya hivi vifuatavyo;
- Mawasiliano (Kuweza kuwasiliana na watu)
- Kuweza kujihudumia katika shughuli zinazohitaji kutumia akili (functional academic skills)
- Kuweza kuishi mazingira ya nyumbani na kazini
- Kuwa na uwezo wa kuchanganyikana na jamii katika masuala ya afya na usalama wake
- Kuweza kutumia huduma za jamii ambazo zitamfanya kuishi maisha ya furaha
Intelligence kitaalamu ni uwezo wa ubongo katika kufikiri, kutatua matatizo, kuchagua au kuwa na busara (reason), na kuelimika.
IQ= Mental age (Umri wa akili) × 100
Chronological age (Umri wa kawaida wa binadamu)
Makundi ya Upungufu wa Akili
Kipimo cha IQ
Upungufu wa akili uliopitiliza kabisa (Profound Mental Retardation) Chini ya 20 Upungufu wa akili mkubwa (Severe Mental Retardation) 20-34 Upungufu wa akili wa kati (Moderate Mental Retardation) 35-49 Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) 50-69 Upungufu wa akili wa kawaida (Borderline Intellectual Functioning) 70-84
Mtu aliye kwenye kundi la upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) anaweza kuelimika, na Yule aliye na upungufu wa akili wa kati, mtu huyu anaweza kufunzwa kazi za kumuwezesha kumudu maisha yake ya kila siku. Wale walio na upungufu wa akili mkubwa (Severe MR) na kundi la waliopitiliza (Profound MR) hawawezi kufunzwa chochote na kufundishika.
Kwa hiyo mtoto aliye na umri sawa wa akili na umri sawa wa kibinadamu atakuwa na kipimo cha akili 100 (yaani IQ=100). Kwa wale watoto wenye vipaji maalum, kipimo cha akili yao huwa zaidi ya 100 (IQ>100), na kwa wale wenye akili ya kawaida kipimo cha akili huwa chini ya 100 lakini hakishuki chini ya 85.
Upungufu wa Akili wa Kawaida (Borderline Mental Retardation)
Huwa na akili yakipimo cha IQ= 70-85%. Wanauelewa mdogo shuleni (Slow learners) lakini wanaishi maisha ya kawaida yaani bila kupata taabu yoyote katika maisha yao ya kila siku na wanaweza kuajiriwa.
Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha IQ=50-70. Asilimia kubwa ya watu wenye upungufu wa akili huwa kwenye kundi hili (asilimia 85-95). Wanatambulika kama wanaoweza kuelimika. Wanaweza kujifunza kusoma, kuandika, na kufanya hesabu rahisi rahisi (simple arithmetic calculations). Hawa wanahitaji shule maalum ili waje kuweza kumudu majukumu yao ya maisha ya kila siku baada ya muda mrefu.Wanakuwa na upungufu mdogo katika uwezo wao wa kuhisi na utambuzi wa vitu (minimal sensorimotor deficits) na ni vigumu kutambua kwamba wanaupungufu wa akili mpaka baadae maishani. Katika ujana wao wanaweza kupata elimu hadi darasa la sita.Ukubwani, hupata uwezo wa kujihudumia wenyewe katika mahitaji yao ya kila siku lakini wanahitaji uangalizi, ushauri, kupewa mwongozo katika majukumu yao ya kifamilia na hasa wanapopata msongo wa mawazo au wakati wamepata matatizo ya kiuchumi.
Upungufu wa Akili wa Kati (Moderate Mental Retardation)
Huwa na akili yakipimo cha IQ=35-50. Asilimia 10 tu ya watu wote wenye upungufu wa akili ndio huwa kwenye kundi hili.Wanatambulika kama wasioweza kufundishika (untrainable) ingawa wengi wao wanaweza kuelimika. Utotoni mwao wanakuwa na mawasiliano mabaya ya kijamii, lakini wanaweza kujifunza kuzungumza, kutambua majina yao na baadhi ya maneno rahisi ambapo kutokana na haya ambayo nimeelezea hapo juu, kwa sasa wanatambulika kama kundi linaloweza kufundishika.Kawaida, huacha shule baada ya kufika darasa la pili (Standard 2). Wanaweza kufundishika katika kazi ambazo hazihitaji kutumia akili ama kazi za mikono.Msongo wa mawazo huathiri mafunzo yao hivyo ni muhimu kuboresha mazingira yao na kuwahudumia vizuri ili wasipate msongo wa mawazo.
Mara nyingi, uwezo wao wa kuelewa watu wanapozungumza ni mzuri kuliko uwezo wao wa kuzungumza na hii huwafanya kupata msongo wa mawazo. Uzungumzaji wao ni wa kawaida na hueleweka vizuri na wale wanaoishi nao au wale wanaofahamiana nao vizuri. Vitendo kama uvaaji nguo, kula, na kujiweka msafi, huchukua muda mrefu kwao kujifunza. Wanahitaji msaada katika matumizi ya hela na hata kuvuka barabara.
Upungufu wa Akili Mkubwa (Severe Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha IQ=20-35 na huonekana kwa watu wenye upungufu wa akili kwa asilimia 5 tu. Hutambulika mapema kwa kutokuwa na uwezo wa kutambua vitu mbalimbali (Poor motor development). Watu hawa hawana uwezo wa kuzungumza na kuwasiliana au hupata uwezo huo baadae maishani. Huitaji shule maalum pamoja na wataalamu wa tiba ya sauti ili waweze kujifunza kuzungumza.Chini ya uangalizi, huweza kujifunza shughuli ndogondogo.
Upungufu wa Akili Uliopitiliza (Profound Mental Retardation)
Huwa na akili ya kipimo cha chini ya 20 yaani IQ<20. Asilimia 1-2 ya watu wenye upungufu wa akili ndio walio kwenye kundi hili. Mara nyingi wanakuwa na ugonjwa au matatizo ya sehemu ya mishipa ya fahamu ambayo husababisha upungufu wa akili.Dalili za kuwa na uwezo finyu wa kutambua na kuhisi mambo mbalimbali, kushindwa kuelimika, kujihudumia, kufanya kazi, kujitunza huonekana mapema sana. Huitaji msaada wa kijamii pamoja na kuhudumiwa katika maisha yao ya kila siku.
Aina za Upungufu wa Akili
Kuna aina mbili za upungufu wa akili ambazo ni;
- Syndromic mental retardation – Hii ni upungufu wa akili (intellectual deficits) unaoambatana na magonjwa mbalimbali pamoja na viashiria na dalili za kitabia (behavioral signs).
- Non syndromic mental retardation – Upungufu huu wa akili hausiani na magonjwa au ugonjwa wowote.
Pathofiziologia (Pathophysiology)
Upungufu wa akili ni mjumuiko wa matatizo katika mfumo wa fahamu (CNS functions) ambapo sehemu inayojulikana kama cortical structures (ambayo huusisha pamoja na sehemu zingine kama hippocampus na medial temporal cortex) ndio huathirika. Watu wengi wenye upungufu wa akili hawaonyeshi kuathirika katika mfumo wao wa fahamu. Ni aslimia 10-15 ya watu wote wenye upungufu wa akili ambao ndio wanaonyesha kuathirika katika mfumo wao wa fahamu.
Matatizo katika mfumo wa fahamu ambayo huonekana sana ni kichwa maji (hydrocephalus), neural tube defects, microcephaly na (disorders of migration- the lissencephalis na muunganiko wa mwatuko wa ubongo {agenesis of corpus carlosum} ambayo huonekana mara chache).
Watu wengi wenye upungufu wa akili aina ya mild mental retardation na wenye matatizo mengine ya ufahamu (other learning disorders), huwa hawana matatizo katika mfumo wao wa fahamu, madhara katika neva na dysmorphisms lakini wana uwezekano mkubwa wa kutoka katika familia zenye hali duni ya kiuchumi, familia yenye kipimo cha akili ndogo (low IQ), na elimu duni.
Nini husababisha upungufu wa akili?
Zipo sababu nyingi ambazo husababisha upungufu wa akili ambazo ni kama ifuatavyo;
- Matatizo ya kurithi (genetic factors)
- Antenatal factors
- Postnatal factors
- Matatizo ya kijamii na kitamaduni (socio-cultural factors)
- Magonjwa ya akili (psychiatry disorders)
Matatizo ya viashiria vya urithi (genetic factors)
- Chromosal abnormalities kama down syndrome, fragile X syndrome (mgonjwa anakuwa na kichwa kikubwa, masikio makubwa kama ya popo, uso mrefu, korodani kubwa kupitiliza na nyayo zinakuwa bapa {flat feet},huwa na matatizo ya lugha na sauti, hii husababishwa na matatizo katika ncha ya mkono mrefu wa chromosome)
- Metabolic disorders kama phenylketonuria, homocystinuri, galactosemia nk.
- Magonjwa kwenye ubongo (Gross disease of the brain) kama cerebral dysgenesis, tuberose sclerosis, neurofibrosis nk.
- Madhara ya kwenye ubongo (brain malformations) kama nueral tube defects, kichwa maji na microcephalus
Antenatal factors
Matatizo ambayo hutokea wakati mtoto bado hajazaliwa (yaani yanayompata mtoto wakati bado yupo tumboni mwa mama yake). Haya yanaweza kuwa;
- Magonjwa kama ugonjwa wa kaswende (syphilis), TORCH
- Sumu (intoxications) kama madini ya risasi (lead), madawa ya kulevya, unywaji pombe wakati wa ujauzito nk.
- Physical damage – Tiba ya mionzi au vipimo vya mionzi, injury, ukosefu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto (hypoxia).
- Matatizo ya kondo la uzazi (Placental dysfunctions) – Toxaemia, ukosefu wa virutubisho sahihi katika ukuaji wa kondo (Nutritional growth retardation).
- Matatizo katika mfumo wa vichocheo mwilini (Endocrine disorders) – Hypothyroidism (ugonjwa wa tezi la koo), ugonjwa wa kisukari kwa mama mjazito, hypoparathyroidism.
Perinatal factors
Matatizo yanayotokea wakati mtoto anazaliwa (wakati wa kujifungua kwa mama mjazito)
- Ukosefu wa hewa ya oksijeni (Birth asphyxia), cerebral palsy nk
- Madhara ya mtoto kuzaliwa njiti (complications of prematurity) kama uvujaji damu ndani ya ubongo (intraventricular haemorrhage).
- Hypoxic Ischemic encephalopathy
Post-natal factors
Matatizo yanayotokea baada ya mtoto kuzaliwa
- Injury – Head injury (kuumia kichwa)
- Sumu (Intoxication) kutokana na madini ya risasi, mercury nk.
- Magonjwa kama ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), encephalitis (maambukizi kwenye ubongo)
Socio-cultural factors (Matatizo ya kijamii na kitamaduni)
Kutokuwa na uwezo wa kujumuika na jamii huchochewa na ukosefu wa elimu, kiwango duni cha uhamasishaji, tabia ya mtu, ucheshi wa mtu,utapia mlo, mimba za utotoni (kwani huleta umaskini, utapia mlo, afya duni, kuathirika kwa mama na hivyo kumuathiri mtoto), vocational opportunities pamoja na magonjwa ya akili na magonjwa mbalimbali. Kukosekana kwa vichocheo hivyo au kuwepo kwa magonjwa ya akili na baadhi ya magonjwa mbalimbali huweza kusababisha upungufu wa akili. Ikumbukwe ya kwamba akili ya mtoto huwa inakuwa kwa hiyo ni muhimu apewe fursa ya kuweza kukuza akili yake.
Magonjwa ya akili (Psychiatric disorders)
- Pervasive developmental disorders (Autistic spectrum disorders)
0 comments:
Post a Comment