Wengi
wetu huchukulia ulaji wa karanga kama chakula cha kujiburudisha na
kisichokuwa na umuhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli
karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama
nitakavyokujuza leo katika makala haya.
nyuma, tuliona
faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa korosho ambapo tuliona ambavyo
mtu anaweza kujiepusha na magonjwa hatari ya moyo na hata kuongezeka
kwa uzito kwa kula korosho tu, halikadhalika karanga nazo zinafaida
zaidi ya hizo.
MAGONJWA YA MOYO
Kama
ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri
aina ya ‘monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa
afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa
mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular
heart disease) kwa asilimia 21.
Aidha, katika taarifa
iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ‘Journal of Nutrition’
ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu
wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa
kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa
zaidi ya asilimia 37.
Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa
kinga kwenye moyo, karanga pia, hasa za kukaanga, zinaelezwa kuwa na
kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants)
kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!
Ili
kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao
unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu,
unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile ‘peanut
butter’, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.
KINGA DHIDI YA KIHARUSI
Ugonjwa
mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au
‘stroke’, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula
karanga tu. Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya
‘Resveratrol’ ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu
(red wine).
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na
kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of
Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho hicho
huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo
kwa kiasi cha asilimia 30.
KINGA DHIDI YA KANSA YA TUMBO
Faida
nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa
karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya ‘folic acid’,
‘phytosterols’, ‘phytic acid’ (inositol hexaphosphate) na resveratrol’
vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa
saratani ya tumbo.
Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa
karanga, hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano
wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia
27 kwa wanaume!
Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga
mwilini, bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika
orodha ya vyakula tunavyokula kila siku na hakika Mungu ametupenda sana
kwa kutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabili kwa njia ya
vyakula.
Monday, 13 October 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment