Na Beatrice Githiri-HLH
Afya na usafi wa kinywa chetu ni muhimu
ili kuboresha mwonekano wetu na pia kutufanya tujiamini. Harufu mbaya mdomoni
hutufanya tusijiamini na pia kutunyima raha ya kucheka au kuongea mbele ya
watu.
Harufu mbaya mdomoni husababishwana:
- Bacteria mdomoni
- Mdomo kuwa mkavu
- Aina fulani za chakula
leo nitazungumzia njia kadhaa ambazo zinaweza kusaidia
kuondoa au kupunguza harufu mbaya mdomoni. Endapo hizi njia hazisaidii ni
vizuri kumwona daktari wa meno kwa ushauri na iba zaidi.
- Piga mswaki baada ya kula
Usafi wa kinywandio namna nzuri
zaidi kupambanana harufu mbaya mdomoni.
- Safisha ulimi
- Unapo swaki ni muhimu kusugua
ulimi kwa kutumia mswaki ili kuondoa bakteria, mabaki ya chakula na’seli’ zilizokufa.
Tafuna bubblish/Big G ambazo hazina sukari
Kwa kutafuna bubblish mtiririko wa
mate huwa mzuri na hivyo kuondoa au kuafisha bakteria, mabaki ya chakula na piahuzuia mdomokuwa mkavu.
Sukutua mdomo mara kwa mara
Kusukutua mara kwa mara huimarisha
usafi wa kinywa na pia kuzuia mdomo kuwa mkavu, hivyo kuepusha harufu mbaya
kutoka mdomoni.
Epuka uvutaji wa sigara
Uvutaji wa sigara hufanya mdomo
kuwa mkavu na hivyo kusababisha harufu mbayakutoka kinywani.
Epuka au punguzavyakula
vinavyosababisha harufu mbaya mdomoni
Vyakula kama vitunguu maji,
vitunguu swaumu, samaki, mayai, kabeji, maziwa husababisha harufu mbaya. Pia
vinywaji kama kahawa na pombe huleta
harufu mbaya haswa kwa watu wenye
mtatizo ya kunuka mdomoni.
Ni matumaini yangu kuwa
somo la leo limekupa ufahamu katika kuboresha afya ya kinywa chako kwa
kuzuia harufu mbaya.
Kiafya tunashauriwa
kumwona daktari wa meno kila mwaka na kama kuna matatizo, angalau miezi mitatu
hadi sita.
Ijue
afya ya kinywa chako kwa kwenda katika huduma ya kinywa na mdomo. Hospitali ya
Kilutheri ya Haydom ina kitengo cha meno na huduma hiyo inapatikana.
0 comments:
Post a Comment