-

-

-

-

-

Habari Mpya

Thursday, 24 July 2014

Jibu la swali la Mdau



Kuna mdau ambaye aliniuliza muda mrefu uliopita iwapo mwanamke na mwanamume ambao wana Ukimwi wanaweza kupata mtoto kwa njia ya IVF au la. Kwa kuwa ni muda mrefu sikuwepo kuandika blog hii na kujibu maswali, nimeamua kulijibu swali hili hapa ili muulizaji aone jibu lake kwa urahisi na wengine pia waweze kufaidika nalo.
 

Jibu ni kuwa ni vigumu kusema kuwa njia hiyo inaweza ku-guarantee kuzaliwa mtoto asiyekuwa muathirika wa HIV, hasa kwa kuzingatia kuwa wote baba na mama ni wagonjwa. Ni kweli iwapo mmoja tu ndiye mgonjwa kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanyika IVF kwa njia inayoitwa Sperm wash ambayo hufanywa kabla ya mbegu ya kiume kutumbukizwa kwenye tumbo la mama na huweza kuzaliwa mtoto asiye mgonjwa wa Ukimwi. 
Lakini sikukatishi tamaa mdau, iwapo huna matatizo ya uzazi, kuna uwezekano wa mwanamke na mwanamume waathirika wa Ukimwi kuzaa mtoto asiyeathirika, iwapo watakuwa wakitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kabla na wakati wa ujazito, na hasa mama kuendelea kutumia dawa hizo wakati wote wa ujauzito.Kuzaliwa watoto wasioathirika kutoka kwa wazazi waathirika wa Ukimwi, kumeshuhudiwa mara nyingi nchini Tanzania na kwingineko.

Kuwaanzisha watoto chakula kigumu miezi 6 mapema kunawasaidia

Maneno haya si yangu, lakini nakumbuka kwa uzoefu wangu siku zote nilikuwa nikipingana na waalimu darasani na mahospitalini kuhusu muda wa kuanzishwa chakula kigumu watoto wanaonyonya au 'weaning'!. Siku zote walimu wangu chuo kikuu walikuwa wakisema kuwa watoto wachanga wanaonyesha waanzishwe vyakula vingine wanapokuwa na miezi minne, lakini mie nikipinga na kusisitiza kwamba muda huo utumike kwa watoto wenye asili ya kizungu au weupe, lakini kwa uzoefu wangu, watoto wetu wa Kiafrika tunawaanzisha chakula kigumu wanapokuwa na miezi minne, kwani ifikapo muda huo maziwa ya mama zao huwa hayawatoshi tena! Pia hata wadau wa Kona ya Afya pale waliponiomba ushauri niliwashauri hivyo.
 
Hoja yangu hiyo imethibitishwa hivi karibuni na timu moja ya Uingereza ambayo ilifanya utafiti na kuchapisha utafiti huo katika Makala ya Tiba ya Uingereza. Wanatimu hiyo wamesema, kutegemea tu maziwa ya mama pekee kwa watoto hadi miezi sita sio vizuri na hayatoshi. Wamesema maziwa ya mama yanaweza kuwa na faida iwapo watoto wataanzishwa vyakula vinginevyo mapema hasa baada ya miezi minne. 
Huko nyuma wataalamu walishauri kuwa mtoto apewe maziwa ya mama pekee hadi miezi sita lakini hivi sasa wamebadilisha msimamo huo na wanashauri mtoto aanze kupewa chakula kingine akiwa na miezi minne huku akiendelea kunyonyeshwa. Miaka 10 iliyopita Shirika la Afya Duniani lilitoa muongozo kwamba, watoto wachanga wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee hadi miezi 6!
 
Utafiti mwingine umeonyesha kuwa, watoto wachanga wanaocheleweshwa kuanzishwa chakula kigumu hupatwa na upungufu wa damu au anemia kuliko wale wanaoanzishwa vyakula vingine wakiwa na miezi minne hadi 6. Hata hivyo wazazi na walezi wametakiwa kuzingatia aina ya vyakula wanavyowapa watoto wao wachanga pale wanapofikia muda wa kuanza kula, kwani baadhi ya vyakula huwasababishia allergies na pia kufanya wakose choo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Jibu la swali la Mdau Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top