-

-

-

-

-

Habari Mpya

Thursday, 17 July 2014

ZIFAHAMU FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI


Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa afya yako, kuna namna mbalimbali za kufanya mazoezi. Unaweza kufanya mazoezi ya viungo fulani vya mwili wako kama miguu, mikono, mgongo nakadhalika. Lakini pia kuna mazoezi ambayo ukifanya utakuwa umefanya zoezi lilojumuisha kiungo zaidi ya kimoja mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo. Licha ya kuwa unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni lakini pia unaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa kufanya mazoezi hayo.
Kwakuwa kuna faida nyingi za kufanya mazoezi basi leo nimeona niorodheshe hizi chache kwa manufaa na ufahamu wa afya yako.
1. Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa shupavu.
2. Mazoezi huboresha ufahamu wako uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.
3. Mazoezi huboresha uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu.
4. Mazoezi husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
5. Mazoezi huimarisha moyo hivyo hukuepusha na maradhi mengi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo.
6. Mazoezi humfanya mtu ajiamini.
7. Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia baridi.
8. Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini.
9. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.
10. Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. (high blood pressure)
11. Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.
12. Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili.
13. Mazoezi huboresha hamu ya mtu kuweza kula.
14. Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.
15. Mazoezi huimarisha mifupa hivyo hupunguza matatizo yatokanayo na kudhohofika kwa mifupa jina la kitaalamu (osteoporosis)
16. Mazoezi huboresha kinga ya mwili.
17. Mazoezi husaidia kuweka sawasawa mifumo mbalimbali ya mwili. Mfano: mfumo wa ufahamu, mzunguko wa damu, homoni na misuli.
Mpendwa msomaji hizi ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, yote ya yote mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya njema. Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli ukifanya mazoezi na kula vyakula bora kunaweza kuboresha maisha yako? 
Jibu ni NDIYO mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika. Fanya mazoezi kuimarisha afya yako!

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: ZIFAHAMU FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top