Wivu
na maumivu anayoyasikia mwanamke pale anapohisi au kugundua kuwa mpenzi
wake wa kiume anatembea nje ya mahusiano yao uko katika kiwango cha
hisia “emotional level”
wakati maumivu anayoyapata mwanaume kwa kusikia au kugundua kuwa mpenzi
wake wa kike anamtu mwingine uko katika kiwango cha himaya “territorial
level”.
Wakati mwanamke anaumia kwa wivu akijiuliza kwanini mwanaume wangu achukuliwe na mwanamke mwingine, huku akiwa na kiu ya kumjua
huyo mwanamke anafananaje? Ananini? Anauwezo gani kimvuto na
kimuonekano? Maswali haya moyoni mwake huongeza maumivu katika hisia za
mwanamke huyu, kwa upande wa pili mwanaume haumii kihisia lakini huumia
na kupata machungu zaidi ya mwanamke huku moyoni mwake akihisi kushindwa
kuimiliki himaya yake vema hadi mwanaume mwingine kuweza kuivamia,
hujihisi kama askari aliye na silaha dhaifu au aliyeshindwa kutumia
silaha zake vema hadi askari wa kambi nyingine akapata urahisi wa
kumvamia tena kwenye kitovu cha kambi yake.
Katika hali hizi, mwanamke humtazama mwanaume wake kama mpenzi wakati
mwanaume akimtazama mwanamke wake kama himaya. Ni ngumu sana mwanaume
kustahimili maumivu ya jinsi hii, na ndio maana kwa wanaume wengine huwa
rahisi hata kuwaza kujitoa uhai au kuutoa uhai wa huyo mwanaume
mwingine aliyetembea na mpenzi wake, wapo pia wanaume ambao huishiwa
nguvu za kufanya tendo la ndoa kwa muda fulani “temporary impotency”mara
tu wanapogundua kusalitiwa, na nimeshuhudia mwanaume aliyeamua kuzikata
sehemu zake zote za siri kwasababu ya kuona hazina tena umuhimu, ingawa
hakuweza kuishi tena baadae.
Maumivu na matendo haya hayafanyiki sana kwa jinsia ya kike, wao huishia
zaidi kulia, kupiga kelele sana, kutukana, na juhudi za kumsaka huyo
mwanamke mwingine zikifanikiwa basi wanaweza kupigana kidogo na
kuwekeana uadui wa kawaida, ambao sikumoja unaweza ukaisha
kwa hisani ya Chrisi Mauki
0 comments:
Post a Comment