Je unamkumbuka
mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson ambaye alikata Uume wake mwezi
Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya hivyo.
Johnson,
aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo chake
cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili. Madaktari
walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua
wiki hii kujieleza kwa nini alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha
televisheni cha E! nchini Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za
kulevya , lakini nilikuwa najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'
Nilikata sehemu
yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu.
Suluhu langu kwa masaiibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha
ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, 'mini ni
mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi.
Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''
Matamshi yake
Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya kiakili,
lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo
jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai, na hilo
ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu. ''
Kwa hisani ya BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment