-

-

-

-

-

Habari Mpya

Thursday, 14 August 2014

Homa ya ini ni ugonjwa hatari kuliko Ukimwi.....


afyatele
Mwanamke akipata chanjo ya homa ya ini, ugonjwa ambao unaua na kusumbua wengi duniani ikiwamo Tanzania. Picha ya Mtandao 


Kwa ufupi Wataalamu wanaeleza kuwa Hepatitis B au homa ya ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi, wenye madhara makubwa na wenye uwezo wa kuambukiza kwa wepesi kuliko Ukimwi.


Ugonjwa wa selimundu unasumbua wengi, umetengua ndoa za wengine, kwa sababu ya kutojua.
Hakuna shaka kwamba umewahi kusafiri nje ya nchi yako na kutakiwa kupata chanjo.

Kwa wengine, chanjo hiyo ikiwamo ya homa ya ini imeonekana kama usumbufu na  udhia mtupu. Hata hivyo, wapo wengine ambao hawaufahamu ugonjwa huu.
Kwa wanaoujua, wanahofia kuwa ugonjwa huu una madhara makubwa pengine kuliko  saratani na Ukimwi.
Homa hiyo au Hepatitis B inapewa uzito mdogo licha ya kuwa ni  ya hatari kubwa.
Wataalamu wanaeleza kuwa Hepatitis B au homa ya ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi, wenye madhara makubwa na wenye uwezo wa kuambukiza kwa wepesi kuliko Ukimwi.
Kitaalamu, ugonjwa huu, husababishwa na virusi vya Hepatitis B (HBV) ambavyo huathiri  mfumo wa utoaji wa sumu mwilini. Inaelezwa kuwa robo tatu ya watu ulimwenguni wameathiriwa kwa muda na homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja kwa moja.
Takwimu zinaonyesha kuwa homa ya ini huua watu 600,000 kila mwaka katika sehemu mbalimbali, idadi ya watu inayolingana na wale wanaokufa kutokana na malaria.
Maradhi haya ya ini yanaelezwa kuwa yanaweza kusababishwa na kunywa kileo kupita kiasi au sumu inapoingia mwilini.
Hata hivyo, mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Wanasayansi kwa upande mwingine wamegundua virusi vitano vinavyosababisha ugonjwa huu na wanasema kwamba huenda kuna vingine vitatu.
Matokeo yake, sheria zimewekwa  katika nchi mbalimbali ambazo zinamtaka kila raia mgeni anayetaka kuingia katika nchi husika, kupata chanjo ya ugonjwa huu ili kuepusha maambukizi.
chanzo Mwananchi
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Homa ya ini ni ugonjwa hatari kuliko Ukimwi..... Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top