-

-

-

-

-

Habari Mpya

Wednesday, 13 August 2014

Shtuka Binti, Hivi Unajua Wanawake Walioachika Wana Visingizio Vingi, Wanawadanganya Wasio Olewa

afyatele
Nimegundua ya kwamba wanawake wengi walio achika katika ndoa zao wana ushuhuda wa uwongo kwa wanawake wasio olewa.

Utamkuta mdada mzima amezalishwa halafu ameachwa kwa makosa yake anawaambia wanawake wasio olewa kwamba kuolewa kitu gani, kwani wewe huwezi kuendesha maisha bila mwanaume, kwani mwanaume nani bwana asikunyanyase , watu tumeona wanaume sembuse magume gume, mwanaume kitu gani bwana, wewe waza maendeleo yako ,usiwaze kuolewa ,kuolewa ni kupoteza muda , kuolewa ni kutiana umaskini tu.

Katika hali isiyo ya kawaida wanawake hao wakipata tena waume wa kuwaoa utaona wanaolewa,halafu cha ajabu hamna shughuri yoyote ya maendeleo wanayofanya zaidi ya kutwa kujadili wanaume za wtu na kuendelea kuzalishwa tu nyumbani.

Waacheni mabinti waolewe na si kuwaharibu kisaikolojia kwamba kuolewa hakuna maana na maana zaidi kuzalia nyumbani kila mtoto na babake. Waacheni kila mtu akaone yeye wenyewe. Kama wewe umeachika wacheni wakajaribu maisha.

Kama una binti yako mzuie kuambatana na akina mama waliotendwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Shtuka Binti, Hivi Unajua Wanawake Walioachika Wana Visingizio Vingi, Wanawadanganya Wasio Olewa Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top