KWA NINI NJIA HII INAFUNDISHWA ?
- Ni njia iliyowekwa na Mungu katika mwili wa mwanamke ambapo ametofautisha siku za uzazi na siku zisizo na uzazi. Wajibu wetu katika ndoa ni kutumia njia hii ama kwa kupata mtoto ama kwa kuahirisha kupata mtoto au kujenga umoja wa miili na mioyo kwa njia ya tendo la ndoa. Mungu ametoa njia hii kama zawadi kwa mwanadamu kwa sababu Yeye anauangalia mwili wa binadamu kama hekalu lake. kwa na kw njia hiyo anamuepusha binadamu na madhara yatokanayo na vidhibiti mamba ambavyo huharibu hekalu hilo
- Ni rahisi kujifunza kwa kujichunguza na kuzitambua ishara za uzazi na zisizo na uzazi ambazo Mungu ameziumba katika mwili wa mwanamke. Wanandoa watumie ishara hizo kwa kupata motto au kuahirisha kupata mtoto
- Hujenga afya ya mwili na roho. Mwanamke anaweza kutambua hitilafu ya afya yake kwa njia ya kujichunguza na hivyo kuchukua tahadhari ya tiba. Mwanamke anaepushwa na msongo wa moyo na anaweza kufurahia tendo la ndoa na kumpokea mwenzi wake kama mshirika wa safari ya maisha yake
- Ni njia yenye uhakika mkubwa ili mradi wana ndoa wazingatie kanuni
- Haina gharama, kwa maana kwamba hakuna fedha zinazo tumika kununua njia hiyo wala hakuna nauli unayo tumia kwenda kuipata.Gharama yake ni NIDHAMU, UPENDO WA KWELI NA KUJITOA KILA MMOJA KWA MWENZAKE, KILA MMOJA KUWA MALI YA MWENZAKE
- Haichafui mazingira; mwili wa mwanadamu hauchafuliwi: ardhi, mimea, maji na anga havichafuliwi kwa sababu hakuna sumu wala kemikali zitupwazo na ziingiazo humo
- Ni njia ya maisha. Wana ndoa wanatumia njia hiyo hadi mwanamke anapokoma kuzaa
- Imetumiwa na watu tangu Mungu alipoweka ndoa ya kwanza ya Adamu na Eva na imekubaliwa na watu wa aina zote na dini zote duniani.
2. Kuna njia nne za kutambua siku za uzazi na zisizo na uzazi
- Kuhesabu siku kwa kutumia kalenda, njia ya zamani ya Dr. Knaus na Dr. Ogino, 1923. Njia hii inaweza kutumika tu na wanawake wanaopata hedhi kwa utaratibu usiobadilika. Njia hii ina hakika ya 66%- 86%.
- Kupima joto la mwili asubuhi, inapanda nyuzi 0.2 – 0.5 baada ya kijiyai kuchopoka (temperature method). Njia hii ina uhakika ya 98. 7% - 99. 5%. Lakini inaweza kuarifu vibaya mama akipata homa kwa sababu ya ugonjwa, k.m malaria.
- Njia ya Billings Ovulation Method (B.O.M) wanawake wote hata wakiwa vipofu wanaweza kutumia. Njia hii ina hakika ya 99%- 99. 5%.
- Wengine wanaunganisha alama ya ute wa uzazi pamoja na kupima joto la mwili asubuhi (Symptothermal Method). Njia hii ina hakika ya 99.2% - 99.8%. Pia inaweza kuarifu vibaya, mama akipata homa.
3. Aina mbalimbali za mwandamo wa hedhi
Mwandamo wa hedhi (menstrual cycle) unaanza siku ya kwanza ya hedhi
mpaka siku moja kabla ya hedhi inayofuata. Kuna mabadiliko mbalimbali
katika mwandamo kama damu, ukavu, ute mzito, utelezi na kubadilika kuwa
tena ute mzito na ukavu. Haya yote yana umuhimu ambao yanaelezwa kwenye
kurasa zinazofuata. Mara nyingi mwandamo una siku 25-34. Wanawake
wengine wana mwandamo mfupi, yaani siku 18-24. Wengine wana mwandamo
mrefu, yaani siku 35-50 au zaidi. Tena urefu wa mwandamo wa hedhi wa
mwanamke mmoja unaweza kubadilika mara kwa mara wakati wa maisha yake.
Tena wengine wanapata hedhi kwa utaratibu, wengine bila utaratibu.
Lakini yote ni ya kawaida, si ugonjwa. Hakuna sababu ya kutumia dawa ya
kurekebisha hedhi, ni maumbile yao. Kinachofanya mwandamo mrefu au mfupi
ni idadi ya siku za kabla ya kijiyai kuiva ziitwazo siku za mapema.
Katika mwandamo mrefu siku hizi ni nyingi. Lakini idadi ya siku kutoka
kijiyai kuiva mpaka hedhi unaanza kila mara ni siku 11-16.
4. Mlango wa tumbo la uzazi na ute wa uzazi
Kijifuko cha kijiyai (Graafian Follicle) kinatengeneza chachu ya
estrogen, inayoingia katika damu. Kiasi cha estrogen kinazidi polepole
kila siku mpaka kinapoanza kuamsha vikunjo vya mlango wa tumbo la uzazi
(cervix) kutengeneza ute wa uzazi. Ute huu unatokea siku moja hata siku
chache kwa mfululizo. Mara nyingi unaanza kuwa mzito na kuzidi kuteleza
na kuwa mwangavu inapokaribia siku kijiyai kinapochopoka (Ovulation)
Alama ya ute huu ni jambo linalofahamika, ni wazi na dhahiri:
Alama ya ute wa uzazi ni kufanana na maji meupe ya yai la kuku
au mlenda, unateleza, unanyumbuka, unavutika mpaka uzi wa sentimeta
chache
Wanawake wanaweza kuushika ute wa uzazi kati ya vidole viwili na
kuvitanua vidole. Kwa njia hii wataona ute huu unavyonyumbuka. Ute wa
uzazi unaweza kuwa mwangavu au mzito kidogo. Rangi yake inaweza kuwa
nyeupe au kimanjano kidogo kwa wanawake wengine ute huonekana
umechanganyika na damu kidogo hasa siku ya kijiyai kinapoiva (Ovulation
bleeding).
Wanawake wanatambua ute wa uzazi hasa kwa kujisikia utelezi kwenye mdomo
wa uke. Kujiskia mkojo au maji ni tofauti. Hata wale wasioona
wanajisikia utelezi huu. Kwa hiyo wanaweza kutumia njia hii kwa kupanga
familia. Wanawke wengine hawaoni ute huu ingawa upo, kwa sababu kiasi
cha ute ni kidogo. Lakini wanajiskia utelezi kwenye mdomo wa uke.
5. Kujiangalia na kuandika
Kwa kutambua siku za uzazi na zisizo za uzazi mama anajiangalia toka
asubuhi mpaka jioni, yaani siku nzima wakati wa shughuli zake za
kawaida.
Je, anaangalia nini?
Anaangalia kama anajisikia utelezi kwenye mdomo wa uke (vulva) au siyo.
Ute wa uzazi unatengenezwa kwenye mlango wa tumbo la uzazi na unashuka
polepole – si kama maji. Ute wa uzazi ukianza kutengenezwa usiku
unakusanyika ukeni. Hautoki, kwa sababu mama amelala. Wakati huu ute wa
uzazi uko ndani ya uke, mama hawezi kujisikia kuteleza, kwa sababu
ndani ya uke hakuna neva inaoweza kupeleka habari ya kuteleza. Akiamka
asubuhi na kutembea, ute huu unaanza kushuka polepole mpaka unafika
kwenye mdomo wa uke baada ya masaa na pengine mpaka jioni saa 11.00 au
12.00. Hapa mama anajisikia utelezi. Jioni mama anaandika alivyotambua
toka asubuhi mpaka jioni. Kwa hiyo mama ana uhakika juu ya ute wake jioni tu
Njia nyingine ya kuangalia ute wa uzazi ni kuona ute baada ya kukojoa.
Lakini mama asitegemee kuona ute. Pengine hawezi kuona ute , kwa sababu
upo kidogo tu, lakini anajisikia utekezi. Kama hakujisikia utelezi wala
kuona ute, anaandika ukavu. Kama alijisikia utelezi hata mara moja tu,
jioni atandika utelezi. Kama ameona ute mzito hata mara moja tu na
safari nyingine ukavu, ataandika jioni ute mzito. Kama ameona damu,
jioni atandika damu.
6. Kazi ya ute wa uzazi unaoteleza na kuvutika.
- Kuchuja mbegu. Mbegu million 400 zinaingia ukeni lakini 200 tu zinapita mlango wa tumbo la uzazi
- Kufunga mbegu za baba katika vikunjo
- Kuzilisha mbegu za baba ili ziweze kuishi siku 3-5
- Kutengeneza mifereji, ili mbegu ziweze kuogelea mpaka kwenye tumbo la uzazi
- Kuyeyusha ute kwa kufungua mlango wa tumbo la uzazi
7. Hali isiyo na uzazi
- Ukavu: maana mama anajisikia ukavu kwenye mdomo wa uke, hana ute.
- Mama anoana kila siku kabla ya kilele ute mzito usiobadilika siku hadi siku kwa wiki mbili na zaidi kwa miandamo mingi. Unaotokea katika mwandamo wa siku 35 au kupungua. Mama ajiangalie miandamo mitatu au zaidi na kuhakikisha, kwamba ute huu haubadiliki. Hapa anaweza kusema, ute huu hauna uzazi.
- Mama anaona aina ya majimaji, pengine meupe kama maziwa yasiobadilika siku hadi siku kwa wiki mbili na zaidi. Haya yanatokana na uke. Yamechanganyika na seli (cells) za ukuta wa uke. Hayana uzazi. Yanatokea katika mwandamo mrefu wa siku 35 na zaidi, kwa mfano wakati wa kumnyonyesha mototo katika hali hizi zote tatu mbegu za baba zinakufa ukeni kabla ya nusu saa.
8. Kiangazi na masika
Tunaweza kulinganisha mwandamo wa hedhi wa mama na misimu ya kiangazi na
masika. Wakati wa kiangazi ardhi ni kavu vile vile, wakati wa masika
ardhi imeloa, nyasi zinaota. Baada ya masika chini bado pamelowa na watu
bado wanapanda kwa muda mfupi. Kwa wanawake wakati wa ukavu hakuna
uzazi, wakati wa ute wa uzazi na siku tatu zinazofuata kuna uzazi.
Ni hivi:
- Ukavu: hakuna uzazi
- Ute wa uzazi na siku tatu zinazofuata zina uzazi
9. Namna ya kutumia BILLINGS OVULATION METHOD
a) Kutatufa mtoto
Fuata kanuni za mapema, ili kugundua mwanzo wa siku za uzazi Kuanza kufanya tendo la ndoa wakati wa kujisikia kuteleza
b) Kupumzika kuzaa
Kujua siku za uzazi na zisizo na uzazi haitoshi kwa kuzuia mimba, bali ni lazima kufuata kanuni za kuzuia mimba.
- Kanuni ya kutokugusana
Kuacha tendo la ndoa kabisa wakati wa siku za uzazi zote, yaani
- Mume asimwage mbegu nje
- Wala mapajani
- Wala kinenani
- Wala kugusana viungo vya uzazi nje, kwa sababu tone dogo la shahawa inaweza kutoka kabla, tena bila mshushio na mbegu zinaweza kuingia katika ute wa uzazi uliopo nje na kuogelea katika mifereji ya ute wa uzazi mpaka ukeni na kwenye mirija na kusababisha mimba.
- Wala kutumia dawa za majira wala kondom siku za uzazi.
- Kanuni za mapema
- Kuacha tendo la ndoa wakati wa hedhi
- Kuacha tendo la ndoa wakati wa damu kidogo na siku 3 baadaye
- Kuacha tendo la ndoa wakati wa ute wa uzazi na siku 3 baadaye
- Kufanya tendo la ndoa siku zisizo na uzazi (ukavu, ute mzito usiobadilika, aina ya majiyasiyobadilika)jioni tu, si kesho yake.
- Jioni tu
Wanaweza kufanya tendo la ndoa jioni tu, kwa sababu jioni mama ana hakika kama ute wa uzazi au siyo. Ute wa uzazi unatoka tu polepole wakati wa kutembea.
- Si kesho yake
Kesho yake anaona shahawa ya mume. Hii inafanana na ute wa mama. Kwa hiyo wakifanya tendo la ndoa kesho yake, mama hawezi kutofautisha kama ute ni wa mume tu au kama mwenyewe ameanza pia kupata ute wa uzazi, yaani mchanganyiko wa ute wa mume na ute wake.
Kanuni ya kilele
Kuacha
tendo la ndoa siku ya kilele na siku 3 baadaye. Kuanzia siku ya nne
baada ya kilele tendo la ndoa linawezekana siku na saa yoyote mpaka
mwisho wa mwandamo.
c) Kutunga mimba kunategemea
- mbegu nzima za baba
- kijiyai cha mama
- mirija mizima
- ngozi nyororo nzima
- ute wa uzazi
- uhusiano mzuri na upendo wa uzazi
Wazazi
wanaotaka mtoto wafanye tendo la ndoa wakati wa siku za uzazi. Wakati
wa siku zisizo na uzazi wafanye tendo la ndoa mara mbili au mara tatu
kwa wiki moja, ili mbegu zipate nafasi ya kuiva.
10. Kuchagua mvulana au msichana
Wazazi wanaweza kuchagua mtoto wa kiume au wa kike kwa hakika ya 85% kwa
njia ya kufanya tendo la ndoa kwa kupanga. Hali ya kuwa -me au -ke
inategemea chromosom X auY ya baba. Katika kijiyai cha mama kuna
chromosom X. Nusu ya mbegu za baba zina chrosom X zinazosababisha kuzaa
msichana. Isitoshe mbegu hizi ni dhaifu kidogo nazo huogelea polepole,
lakini zinaishi muda mrefu. Nusu ya pili ya mbegu za baba zina chromosom
Y zinazosababisha kuzaa mvulana. Isitoshe mbegu hizi ni zenye nguvu,
huogelea upesi na kufa upesi. Kuchagua mtoto wa kike au wa kiume ni
lazima mwanamke ajue ute unaovutika na kuteleza.
a) Kuchagua mvulana
Wazazi wafuate kanuni za mapema, yaani waanze kufanya tendo la ndoa siku
ya kwanza baada ya kilele na kuendelea. Wafanye hivi kwa miandamo 6 ya
hedhi. Kama mama hajapata mimba baada ya miandamo sita, wazazi waanze
kuona siku ya kilele na siku ya kwanza baada ya kilele. Kama mama
amekosa siku ya kilele, yaani kama utelezi unaendelea siku inayofuata.
Kwa njia hii mbegu za chromosom Y tu zitafika kijiyai kilichopoka, kwa
sababu mbegu za chromosom X zinaogelea polepole tu.
b) Kuchagua msichana
Wazazi wafuate kanuni za mapema na kufanya tendo la ndoa siku ya kwanza
ya ute wa uzazi. Halafu wasionane mpaka siku ya nne baada ya kilele.
Waendelee hivi kwa miezi michache.
Kama mama hajapata mimba baada ya miezi michache waonane siku ya kwanza
na ya pili ya ute wa uzazi halafu wasionane mpaka siku ya nne baada ya
kilele. Waendelee hivi hivi kwa miezi michache.
0 comments:
Post a Comment