Vijana
wengi wa kiume hujikuta katika wakati mgumu kuchukua maamuzi ya kuishi
na mwanamke japo yawezekana wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa muda
mrefu kutokana na vikinza vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na
vingine ni nadharia tu.Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa.
2.Utitiri wa wanawake wanaopatikana kirahisi bila hata kuoa (Kwa kimombo hujiambia, “If I can get it for free, why buy it?”)
3.Maradhi hasa ugonjwa wa UKIMWI (Wengi hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa)
4.Kufurahia ‘uhuru’ [Hawa ni makapera wazoefu (wengine husema ‘bachela
sugu’), hakuna mtu ambaye anaweza mshawishi akabadilisha maisha yake
hayo ya kikapela (bachelor)]
5.Uhaba wa wanawake wanaofaa kuolewa
6.Kutopata ampendaye kwa dhati
7.Mahusiano mabovu ya awali
8.Kutoridhika na kipato chake (Hapa namaanisha pale ambapo mwanaume ana
uwezo kabisa wa kuwa na mke na pia kuweza kukimu mahitaji yote pamoja na
ya familia yake).
Malezi na Makuzi
1.Dhana mbovu juu ya ndoa (Kumekuwa na tabia ya watu kukatisha tamaa kwa
kutoa vigezo, sababu, hadithi juu ya ndoa ambazo ni za kubomoa kuliko
kujenga.)
2.Kuzaa ovyo/Kuzaa kabla ya ndoa (Kuna wanaume hadi anafikia umri wa
miaka 30 tayari ana watoto wa wanawake tofauti hata watano na analea)
3.Kukua kwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa (Ni wanaume wachache
wana kifua cha kuweza kuvumilia mkewe/mpenziwe kutoka nje na kuendelea
kuwa naye)
Naomba tuungane katika mjadala, kupata mawazo zaidi, maoni, marekebisho
na mengine mengi ambayo yanaweza kuwa msaada kwa mada hii.
Mdau - AshaDii.
0 comments:
Post a Comment