![]() |
Mmea wa bangi |
Kuna hatari Taifa letu la Tanzania
kugeuka kuwa jalala na hodi za waathirika wa dawa za kulevya,
tusipokubari kufanya maamuzi ya busara katika kuishauri jamii kuacha na
kuepuka kutumia dawa za kulevya.
Mpendwa msomaji kuna aina mbali mbali
za dawa za kulevya zenye athari nyingi na kubwa katika miili yetu,maisha
yetu na hata vizazi vijavyo iwapo tukiendelea kuto wasaidia waathirika
wa dawa hizo za kulevya. Kwa mfano kuwapa ushauri kuweza kufika katika
zahanati zilizokaribu ili kuanza tiba mapema.
Sii mimi peke yangu ambaye
ninashuhudia waathirika wengi wa dawa za kulevya wanavyo pata tabu bali
kila mtu anajionea kinachoendelea katika Taifa letu.Waathirika wengi
hutengwa na ndugu na jamaa, marafiki na hata majirani, baada yakuwa
wamekwisha poteza mwelekeo wa utimamu.
Watu wamekuwa wakishindwa kufahamu kuwa mara tuu unapo anza kutumia dawa za kulevya ndipo unapokuwa unaanza kuathirika kiafya.
Isipokuwa mwanzo huwezi kutambua kuwa unaathirika au la.Kuna dawa nyingine huchukuwa muda mrefu kuonyesha dalili, ila unashauriwa kujitambua kiafya mara kwa mara kwa kufanya vipimo vya mwili wako katika hospitali iliyoko karibu na wewe.
Isipokuwa mwanzo huwezi kutambua kuwa unaathirika au la.Kuna dawa nyingine huchukuwa muda mrefu kuonyesha dalili, ila unashauriwa kujitambua kiafya mara kwa mara kwa kufanya vipimo vya mwili wako katika hospitali iliyoko karibu na wewe.
Bangi.
Bangi ni mmea ulio na asilimia kubwa
ya watumiaji kulingana na takwimu za afya zinavyo onyesha.Mmea huu una
rangi ya kijani ambao hutoa majani, maua na mbegu ambazo hutumika kama
kilevi. Bangi hustawi karibu maeneo yote hapa nchini na hutumika zaidi
kuliko dawa nyingine za kulevya.
Kulingana na matukio, takwimu za afya
zinaonyesha kuwa bangi hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara,
Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Tabora, Kagera na Mbeya.
Pia bangi hujurikana kwa majina mbali mbali kama, msuba,ganja, daga, jani, stiki, ndumu, kaya, msokoto na kadharika.
Pia bangi hujurikana kwa majina mbali mbali kama, msuba,ganja, daga, jani, stiki, ndumu, kaya, msokoto na kadharika.
Mvutaji wa bangi hubakiza moshi mwingi
kwenye mapafu kwa muda mrefu,moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu
hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa
mapafu.
Madhara:
Bangi husababisha madhara mbali mbali
ikiwa ni pamoja na kuumwa koo, kupata kikohozi na saratani ya mapafu,
kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye
mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.
Bangi pia hupoteza kumbu kumbu,
kuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi, uhalifu na kadharika. Pia kuna aina
nyingi za sura tofauti za bangi kwa mfano, kuna mafuta ya bangi, bangi
kavu na bangi iliyo sindikwa.
Mirungi:
Pia kuna aina nyingine ya dawa ya
kulevya ambayo huwa na majina mengi ya mtaani kama “Miraa, mbaga,
mogoka, veve, mogoka, gomba, kashamba” n.k
“Mirungi ni aina ya mimea inayostawi
kwenye hali ya unyevu nyevu na milima yenye urefu kati ya futi 4000
hadi 9000. Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili
katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga, hata hivo
kulingana na uchunguzi mirngi mingi itumikayo nchini kwa kiasi kikubwa
hutoka nchini Kenya.
Madhara:
Kuna madhara mengi ya kiafya na
kisaikolojia pia ambayo huwakumba watumiaji wa mirungi, mojawapo ya
madhara hayo ni matatizo ya kisaikolojia kama, ukatili, kukosa hamu ya
kula, vidonda vya tumbo na vindonda vya mdomoni, kupungukiwa maji
mwilini, shinikizo la damu, maumivu makali ya kichwa, kuharibika kwa
Ini.
Mirungi husababisha mtumiaji kukosa
usingizi kwa muda mrefu hivyo kuongeza uwezekano wa kupata ajali,
wanafunzi kushindwa kuelewa masomo. n.k.
Heroin:
Heroin ni aina ya dawa ya kulevya itokanayo na mmea unaojulikana kama “Opium poppy”dawa hii hupumbaza mfumo wa fahamu.
Kwamujiu wa ripoti za taasisi za afya
zinaonyesha kuwa Heroin huingizwa nchini ikitokea nchi za mashariki ya
mbali kama Afghanistani, Pakistan, Thailand, India n.k.
Dawa hii pia ina majina mengi ya mitaani kama Unga, Brown sugar,Ngoma,Ubuyu,Mondo, Panda, Dume Farasi n.k.
Matumizi:
Heroin hutumika kwa kuvuta, kunusa
unga, kunusa moshi na kujidunga sindano.Kuna madhara mengi sana
yatokanayo na utumiaji wa dawa hii aina ya “heroin” ambayo
asilimia 100 hutoka katika nchi za ughaibuni, madhara hayo hujitokeza
katika mengi kama, mtumiaji mwenye ujauzito na madhara ya kijamii kawa
ujumla.
Madhara:
Mdhara hayo ni pamoja na kuharibika
kwa mfumo wa ubongo na fahamu, mabadiliko ya hedhi kwa wanawake, kushuka
kawa mapigo ya moyo, kupata kizungu zungu, kichefu chefu na kutapika,
dozi kuwa husababisha kifo, mchanganyiko wa heroin na pombe huleta
madhara makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kifo cha ghafla.
Utumiaji wa heroin kwa njia ya kujidunga sindano husababisha maambukizi ya “Virusi vya Ukimwi” (VVU) na magonjwa mengine ya damu kutokana na kushirikiana sindano na vifaa vingine.
Madhara mengine ni kwa watumiaji wenye ujauzito, ambayo ni kupata
matatizo ya moyo, upungufu wa damu, mamba kuharibika, kuzaliwa watoto
njiti, watoto kupata matatizo ya kiafya ikiwemo kuchelewa kukuwa kiakili
na kimwili pia kujifungua watoo ambao mara nyingi hufa wakiwa chini ya
umri wa miaka mitano.
Tumbaku
Uvutaji wa tumbaku una uraibu mkubwa. katika nchi zilizostawi kiviwanda, ni muuaji namba moja na unaendelea kutishia afya ya binadamu ulimwenguni kota. Hii ndiyo bidhaa ya pekee inayopatikana kihalali kote duniani ambayo hudhuru afya ya binadamu ikitumiwa ilivyokusudiwa. Aidha, inajulikana kwa kusabibisha vifo vingi kuliko vileo vyote vinavyoamsha akili.
Ni tatizo la afya muhimu sana linalozuilika katika nchi zilizoendelea. kama tukiendelea na mtindo huu wa sasa, vifo kutokana na tumbaku duniani kote vinatarajiwa kufikia milioni kumi kila mwaka au zaidi ya asilimia kumi ya vifo vyote duniani itimiapo robo ya pili ya karne hii.
Utumiaji wa tumbaku na wanawake wajawazito waweza kuzua matatizo yanayohusiana na mimba, kupunguza ukuaji wa mimba yenyewe, uzani mwepesi wakati wa kuzaliwa, kuzaliwa kwa watoto kabla ya kufikisha muda wao, kuharibika kwa mimba, watoto kuzaliwa wakiwa wafu, watoto kufa wazaliwapo na vifo vya watoto wachanga. matokeo ya kudumu kwa mtoto mchanga ni kama kudumuza ukuaji wa mwili na akili wa mtoto.
Ushahidi wa hivi majuzi pia ulithibitisha kuwa uvutaji hudhoofisha kinga mwilini na hivyo kutia hatarini zaidi kinga ya wavutaji tumbaku wenye virusi vya UKIMWI.
Kwa sasa uvutaji tumbaku unasababisha asilimia tisini ya saratani ya mapafu, ambayo ni asilimia thelathini ya saratani zote zikiwekwa pamoja. Zaidi ya asilimia themanini ya ugonjwa sugu wa kifua pamoja na asilimia ishirini hadi ishirini na tano ya magonjwa yote ya moyo na kupooza husababishwa na uvutaji tumbaku.
Wasiovuta kama vile watoto, wanapovuta moshi wa sigara katika chumba kisichoingiza hewa safi wakiwa na mvutaji huweza kupatawa na magonjwa ya matatizo ya kupumua, hasa kwa watoto.
Kokein
Mmea wa koka (trythroxylon coca) ni gugu lisilokauka lipatikanalo kwa wingi katika maeneo ya Marekani kusini mwa Mlima wa Andes. Kiungo chake tendaji ni alkaloid cokeini, uvumbi mweupe utolewao katika majani yake kwa njia urahisi. Kokeini ni dawa yenye matokeo ya uchachawishi.
Utumiaji wa koka ulikuwa mazoea ya jadi katika baadhi ya maeneo ya tamaduni za kihindi katika Milima ya Andes. Hutumika kama chachawishi, ikiongeza nguvu stahimilivu za mwili na akili huku ikimaliza hamu ya kula na kunywa.
Utafunaji wa matawi ya koka ulijulikana pia kuwa una sehemu muhimu katika shughuli za mila na sherehe za baadhi ya makabila asili ya Marekani kusini, ikichachawisha ukariri wa mkusanyo wa visasili na ufufuaji wa kumbukumbu za kihistoria kupitia usimulizi wa hadithi.
Ukuzaji haramu wa kokeini duniani umeongezeka maradufu kati ya miaka 1985 na 1994. Jambo hili limesababisha ongezeko la biashara ya mihadarati na hivyo kueneza dawa hiyo katika maeneo mapya ya kijiografia hata kufikia sehemu za Afrika.
Uvumbi wa kokeini hutumizwa kwa njia ya kunisisha puani. Aidha, uvumbi waweza kupashwa na kugandishwa kuwa dutu ngumu yanye nguvu zaidi iitwayo kokeini 'ceack', ambayo yaweza kuvutwa kwenye kiko au kuyeyushwa majini na kudungwa kwa sindano.
majani ya koka yanaweza kutafunwa peke yake lakini zoezi hili halifanywi na watumiaji nje ya wakazi asili wa tamaduni za Marekani kusini.
Dawa hii nguvu kubwa ya kusababisha utegemezi wa kisaaikolojia na kimwili. Utegemezi wa kimwili utakuwepo, kama kokeini imettumiwa katika viwmango vikubwa kwa muda mrefu.
Utumiaji wa mwanzo wa kokeini husababisha na 'utmamu usioelezeka' unaofuatwa na wingi wa raha, ambayo hudumu kati ya dakika 30 hadi masaa machache kulingana na kipimo kilichonisishwa.
Watumiaji huripoti hisia za hali ya juu ya nguvu stahimilivu za akili na mwili, utambuzi wa hali ya juu, hisia za kujionea fahari, mwenye uwezo na mara nyingine wasiwasi au wazimu wa kufikiria unaonewa kila wakati.
Baada ya hisia hizi kupungua, mtumiaji wa kokeini huweza kupatwa na mahangaiko, wasiwasi, mfadhaiko, kuwa katika hali ya kukasirika, kutokulala na shauku ya kutaka kokeini zaidi. matukio ya uchokozi yameripotiwa kwa watu kama hawa. Watumiaji wabaya waliozoea hupatwa na njozi.
Utumiaji vibaya sugu wa kokeini humfanya mtumiaji vibaya kujifikiria mwenyewe, na hujulikana katika utmaduni wa vileo kama dawa ya "kujipenda".
Hivi ndivyo dawa hizi hatari za kulevya yani Bangi, Mirungi, naHeroin zinavyo athiri Taifa letu linalo tumia motto “hali mpya nguvu mpa na kasi mpya”
Kila kitendo kinacho enda kinyume na jamii huwa kina kiuka sheria ya
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo utumiaji wa dawa za kulevya ni
makosa kisheria na sheria hiyo huhusika kudhibiti utumiaji, uuzaji,
usafirishaji, uhifadhi au utengenezaji wa dawa za kulevya ni kosa la
jianai.Adhabu kwa mtumiaji, mtengenezaji au msafirishaji atakayebainika
hufikia hadi kifungo cha maisha.
Watanzania wenzangu tushirikiane na taasisi mbali mbali nchini ili
tuweze angalau kulinusuru Taifa letu na vizazi vijavyo kuto athirika na
dawa hizi ambazo zimeenea dunia nzima.
0 comments:
Post a Comment