-

-

-

-

-

Habari Mpya

    Wednesday, 13 August 2014

    UKATILI WA KIJINSIA

    afyatele
    Mwanamke akipigwa na Mwanaume.



    Kasi ya ukatili wa kijinsia nchini tanzania hivi sasa umeongezeka sana kutokana na wananchi wengi kutofahamu elimu ya kisheria zinazosimamia makosa hayo.

    dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Dodoma la Afnet, Sara Mwaga, alisema hayo kwenye warsha ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Singida juu ya vitendo hivyo, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). 



    Alisema kuwa ukatili wa kijinsia ni vitendo anavyofanyiwa mtu vinavyomuumiza kimwili, kiakili, kisaikolojia au kiroho na kiutu.

    Kwa mujibu wa Mwaga aina za ukatili ni pamoja na kupiga, matusi, dharau, kubaka, kulawiti, kashfa na kusingizia.

    Alisema kuwa zaidi ya wanawake milioni mbili hukeketwa kila mwaka duniani wakati kwa Tanzania ni asilimia 18 ya wanawake wote.

    Hata hivyo, Mwaga alisisitiza pia kuwa utafiti unaonyesha kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake wote wameshawahi kubakwa, kupigwa, kulazimishwa ngono au kunyanyaswa kwa njia moja au nyingine katika maisha yao.

    Alifafanua kuwa Umoja wa Mataifa na jumuiya nyingine za kimataifa kwa mfano Umoja wa Afrika, SADC na vyombo vingine pia vimetoa matamko na mikataba mbalimbali inayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

    “Mikataba na makubaliano haya yamekuwa yakitaka nchi wanachama kutunga sera na sheria zinazopinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutekeleza kwa vitendo sera na sheria hizi,” alisisitiza.

    Alisema Tanzania imeridhia mikataba hiyo na imetunga baadhi ya sera, sheria na mikataba ya kitaifa ya kupambana na ukatili wa kijinsia, ingawa bado vitendo hivyo vinaendelezwa katika kila eneo la nchi.

    Wakichangia mada ya elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia, washiriki wa warsha hiyo waliweka wazi sababu zinazochangia vitendo hivyo kuwa ni pamoja na uchumi au umaskini, ushirikina, mila na desturi na ukosefu wa elimu.

    Sababu zingine ni makuzi mabaya ya malezi, sera na sheria kandamizi, mmomonyoko wa maadili, ulevi na dawa za kulevya, utandawazi, mfumo dume, kufuata mkumbo, ubinafsi, tamaa, vita na ulipaji wa mahari.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UKATILI WA KIJINSIA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown