Wanaume
12 wamejikuta wakilazimishwa kutaihiriwa bila ridhaa yao hivi karibuni
nchini Kenya. Wanaume hao wa jamii za Wajaluo, Turkana, Iteso na Luhya
walivamiwa katika mji mdogo wa Moi Bridge, huko Rift Valley na
kulazimishwa kufanyiwa tendo la tohara wikiendi iliyopita baada ya
fununu zilizokuwa zikizunguka kuwa hawajatahiriwa.
Kwa mujibu wa mtandao Daily Post nchini humo ulioripoti jumatatu tarehe 4, wake za wanaume hao 12 waliamua kuvujisha siri za ndani za waume zao baada ya kulalamika kuwa hawaridhishwi katika tendo la ndoa na kwamba kuna hali ya uchafu mwingi katika maumbile ya waume zao.
Wanaume
hao ambao wengi wao ni madereva na makuli walijikuta katika wakati
mgumu baada ya kulazimishwa kushusha suruali zao hadharani na kuanza
kufanyiwa upasuaji huo mbele ya kadamnasi bila ganzi ili kupunguza
maumivu.
Mwanamke
mmoja aliyejitambulisha kama Ann Njeri, aliliambia gazeti hilo kuwa
anafuraha kwamba mumewe amefanyiwa tohara kwani sasa ataanaza kufurahia
uwezo mpya na kwa usafi katika tendo la ndoa katika ndoa yake.
Wanaume
waliotekeleza kitendo hilo walidai kuwa shughuli hiyo itaendelea katika
eneo hilo mwenzi mzima wa Agosti, mwezi ambao ni msimu wa tohara, ili
kuhakikisha wanume wote wana kamilika kutoka kwenye uvulana kuwa
wanaume.
Watahiriwa
hao 12 walipewa kiasi cha shilingi 3000 za Kenya (sawa na shilingi za
Kitanzania 56,584) kwaajili ya matibabu na chakula chenye virutubisho
muhimu, ili kupona haraka. Wakati huo huo zaidi ya wanaume 50 ambao
hawajatahiriwa wanaoishi katika mji wa Daraja la Moi wamepiga kambi
katika kituo cha polisi wakihofia kutahiriwa kwa nguvu kama marafiki
zao.
Source:paparazihuru.com
0 comments:
Post a Comment