KUNA mjadala
mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti
wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi
kiafya kuliko hata sigara!
Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika
masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi
yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya
kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.
Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima,
yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa
wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa
mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa
mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa
‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn
syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari,
ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi
hivi sasa na dunia kwa ujumla.
Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba
mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu
anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali
ndiyo ukweli halisi”.
Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya
kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo
inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari
kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila
shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu
wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda
ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!
Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una
madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku,
utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa
na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!
‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango
kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida.
Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia
kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda.
Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote
wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa
soda!
Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara
kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata
hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15
kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na
magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).
Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko
wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na
asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni
karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.
Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo
la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii
kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara
kwenye ini kama inavyofanya pombe.

Saturday, 11 October 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment