"Mimi ni mwanamke wa miaka 28
nimeolewa na nina 2 beautiful kids. Tatizo langu ni kuwa, toka nimezaa
mtoto wa kwanza miaka 12 iliyopita huku kwenye Uke kunatoka udenda
mweupe unanuka sana hata kama nikimaliza kuoga najiingiza vidole
kujisafisha lakini harufu ipo pale pale na nikikaa na mtu karibu nahisi
kabisa wanaisikia harufu yangu.
Mume
wangu huwa namuuliza unasikia harufu huwa anasema hunuki hata kidogo
ila naona anaogopa kuniambia labda nitakasirika huwa naona aibu sana
kulala na mume wangu maana ni harufu kali mda wote lazima nivae pad la
sivyo chupi yote inakua mbichi pia wakati wa kufanya mapenzi najaa sana
maji hadi sijisikii kufanya na mume wangu pia nahisi labda na magonjwa
sijui nifanye nini yani sina raha ....
(Admin; Unaweza kuipost hii ili kama kuna mtu alishawahi kupata tiba anisaidie) thanks."
Jawabu: Ewe mdada wa miaka 28, kwanza pole na tunatoa shukrani kwa ufafanuzi. Ingekuwa ute mweupe
mzito kama "cream" au laini kama "Lotion" (inategemea na mzunguuko wako
kwa wakati huo) ningesema ni Utoko lakini "udenda" mweupe na wenye
harufu ni wazi kuwa baada ya kujifungua ulipata maambukizo.
Kwakweli
hapa nakushauri ukamuone Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa
ushauri na hatimae matibabu, huenda tatizo halipo kwenye uke bali ndani
kabisa kwenye viungo vya uzazi. Tafadhali fanya mihadi na Mtaalamu wa
magonjwa ya akinamama, hasa wazazi kwa ushauri zaidi.
Ikigundulika
unatatizo basi ni vema kama utamshauri mumeo pia apate matibabu kwani
asipopata matibabu atakuambukiza tena kile alichonacho ambacho amekuwa
akikutana nacho kila mnapofanya mapenzi.
Kumbuka
kuwa wanawake huwa wana vijidudu marafiki ambavyo vinaishi ndani ya Uke
lakini vikikanganywa kidogo kutokana na mabadiliko ya mwili wako,
madawa, lishe n.k. vinaweza kukasirika na kusababisha ugonjwa maeneo
hayo.
Vilevile kuna
magonjwa mengine ya zinaa mtu anakuwa nayo kwa muda mrefu bila dalili
yeyote na baadae ndio unakutana na matatizo kama hayo ya harufu, kuumwa
tumbo n.k. Ni vema tukawa na tabia ya kupima magonjwa ya zinaa mara kwa
mara kwani mengine hujitokeza yenyewe tu kutokana na "friendly bacteria"
ambao kama nilivyosema wanawake wanavyo, wasipokuwa makini na "life
style" au usafi wanaweza kuambukiza wenza wao.
Tunashauriwa
mara chache wanandoa kutumia Condoms na kuangalia magonjwa ya zinaa
mara kwa mara.....tendo la Ngono (yaani ile Uke kukutana na Umme)
inaweza kusababisha mkanganyano wa wadudu marafiki wa ukeni na kuibua
gonjwa la zinaa.
Kila la kheri huko kwa Dokta!!!
Monday, 13 October 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment