KARIBU katika safu ya makala ya afya, ili tuweze kufahamu mengi
kuhusiana na afya zetu na hatimaye tujue jinsi ya kujikinga, ili
tusipate magojwa mapya na matibabu kwa ujumla.
Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya uzazi, hivyo nimeona leo bora tuelimishane kuhusiana na tatizo la ugumba.
Tutaangalia ugumba kwa mwanamke na pia tutaangalia njia za kupata matibabu na kumaliza kabisa tatizo hili.
Maana ya ugumba
Ugumba ni hali ya kushidwa kupata ujauzito kwa mwanamke, lakini
wakati huo huo akishidwa kupata ujauzito wakati anashiriki tendo la ndoa
vizuri kwa muda mrefu takribani mwaka mmoja akiwa atumii kinga yoyote.
Kwa maana nyingine anashiriki akitarajia kupata kupata mtoto, lakini hapati ujauzito ndipo mwanamke huitwa mgumba.
Tatizo hili la ugumba limegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni
(Primary Infertility) hii ni mwanamke ambaye hana historia ya kupata
ujauzito na sehemu ya pili ni (secondary Infertility) hapa mwanamke
anakuwa tayari huko nyuma alishawahi kupata ujauzito, haijalishi alizaa
au mimba iliharibika.
Sababu za ugumba
Ovulatory
Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai (Ovulatory).
Hili ndilo tatizo la kwanza ambalo linawaathiri wanawake wengi kwa kiasi
kikubwa.
Mwanamke anapata siku zake kama kawaida, lakini hapevushi mayai , hii
husababisha na matatizo ya homoni mwilini. Tatizo linaweza kutokea
lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwili.
Wingi au uchache wa homoni
Tatizo jingine ni wingi au uchache wa homoni huchangia kukosekana kwa
mayai yaliyopevushwa kipindi fulani na husababisha mwanamke kushidwa
kupata ujauzito.
Kuharibiwa kwa kizazi
Kuharibiwa kwa kizazi kwa namna moja au nyingine huweza kusababisha kuwa
mgumba. Kwa mfano kuna baadi ya wanawake huathiriwa na bakteria ambao
hawana madhara yoyote, lakini wanapoongezeka au kuzidi kutokana na
matumizi ya antibiotic huathiri mfumo wa kizazi kwa mwanamke.
Pelvic inflammatory disease
Kitu kingine ni (Pelvic Inflammatory Disease) ambalo husababishwa na
maambukizi ya magojwa ya ngono ambayo yakikushambulia sana basi baadaey
unaweza kuwa na tatizo la PID ambao huenda kuathiri ukuta wa kizazi,
hivyo inakuwa ngumu mimba kushika na hivyo kuwa mgumba.
Mayoma
Tatizo la Mayoma ni uvimbe ambao hautokei kuwa saratani hunaweza
kusababisha mwanamke kuwa mgumba. Kwa kawaida uvimbe huu huwa
unajiotesha katika ukuta wa kizazi na huendelea kukua ndani ya ukuta wa
kizazi na kadri uvimbe unavyozidi kukua basi kitoto hushidwa kukua.
Sababu nyingine ni kugeuka kwa kizazi au kizazi kukaa upande. Pia
huweza kuchangia kwa asilimia kubwa mwanamke kushidwa kupata mimba.
Kuziba kwa mirija
Umbo la mirija ya uzazi ya mwanamke huchangia mwanamke kuwa mgumba. Kwa
kawaida, ili mwanamke aweze kupata mtoto ni lazima yai lake liweze
kusafirishwa kwenda kwenye mji wa mimba kupitia mirija ya (Fallopian
tube) na ikitokea fallopian tube imeziba au kuharibika kuna vitu vingi
hutokea sababu ule uharibifu unaotokea kwenye ule mrija kukaharibika
viungo hai vilivyo katika mirija hiyo huweza kusababisha mimba kutungia
nje ya kizazi na huweza kuondolewa kwa mrija ambao una hitilafu, hivyo
mtu huweza kupata ugumba.
Msongo wa mawazo
(Emotional stress) kuwa na msongo wa mawazo husababisha (homon inbalance) ambayo huasababisha mayai kushidwa kukomaa.
Matumizi ya kemikali
Matumizi ya vitu vyenye kemikali nyingi huweza kusababisha homoni
kutokuwa sawa na kupelekea shida ya kutokukomaa kwa mayai na kusababisha
ugumba.
Mpangilio mbaya wa chakula
Diet mbovu na mazoezi kupita kiasi huweza kusababisha tatizo la ugumba
bila mwenyewe kujijua na pia matumizi ya sigara kupita kiasi huweza
kusababisha tatizo la ugumba.
Hivyo, wanawake hushauriwa kutokujinyima kula kisa kupunguza mwili au kufanya mazoezi kupita kiasi, ili tu kupunguza mwili.
Dalili za ugumba
Dalili ya kwanza ukiona uko katika mahusiano au ndoa na unashiriki
tendo vizuri kwa muda usiopungua mwaka mmoj, hutumii kinga ya aina
yoyote na bado hupati ujauzito, basi jua inawezekana ukawa na tatizo la
ugumba.
Pia ukiona siku zako za hedhi haziendi vizuri tarehe zake zinapishana
pishana sana na hupata maumivu makali, basi yawezekana ukawa na
matatizo ya ugumba.
Kupata maumivu makali chini ya kitovu upande wa kulia na kushoto kwa
ndani yawezekana una tatizo hilo sababu. Dalili hizi huashilia kuwa na(
ovarian cyst) au ukawa na shida katika mirija ya uzazi.
Dalili nyingine ukiona mwilini wako una manyonya mayonya au ndevu kifuani hiyo nayo ni moja ya dalili za ugumba.
Kushidwa kushiriki tendo la ndoa au kutofurahia tendo la ndoa huenda ukawa uko mbioni kupata tatizo hilo.
Ushauri
Kwa mwanamke ambaye amepatwa na tatizo hili anashauriwa kuwaona
wataalamu, ili kupatiwa matibabu na kumaliza tatizo hili . Kwa wewe
mwanamke ambaye hujapatwa na tatizo hili, jitahidi kujikinga, ili
usipate, pia epuka vitu vyote ambavyo huweza kukusababishia tatizo la
ugumba.
Matibabu
Kwa kawaida matibabu hutegemea tatizo limefikia wapi na matibabu hufanyika baada ya kuwaona wataalamu.
Kwa mawanamke ambaye unasumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu
nakushauri ukawaone wataalamu au kama umeshaonana wa madaktari na
hujafanikiwa fika Foreplan Clinic iliyopo Ilala-Bungoni, ili uweze
kupata tiba mbadala na kuondokana na taitizo la ugumba.
Na Dk. Juma Mwaka
Friday, 31 October 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment