1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo
hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu.
Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito.
2. Samaki
kutoa baharini, asa wenye magamba ambao huwa na virutubisho vya zinc
vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu za kiume.
Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kuku huwa na kiasi kikubwa cha madini haya.
3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia kuondoa
mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya
moyo.
4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia.
5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo
husaidia kujenga misuli imara. Pia ina bacteria rafiki wanaosaidia
kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo. 6. Ndizi mbivu, Ina virutubisho vya potassium ambavyo uimarisha misuli, mifupa na kupunguza shinikizo la damu.
7. Nafaka, vyakula hivi huongeza nguvu na huwa na nyuzinyuzi kusaidia kupata choo vizuri na kuimarisha mwili wako.
8. Tomato Souce ina virutubisho vya leukopene ambavyo ukulinda dhidi ya saratani ya tezi ya kiume.
9. Mboga za majani na matunda, kama
pilipili, machungwa, karoti, spinachi na maboga zina kemikali na
virutubisho vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili, kuzuia kuzeeka mapema
na kukukinga na saratani.
10. Mayai, yana virutubisho vya lutein, protini namadini ya chuma yanyosaidia ukuaji wa chembe nyekundu za damu.
Monday, 13 October 2014
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment