Madaktari
nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana
Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya
kinywani .
Dr Sunanda
Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini
Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa
Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika
kwa maumivu makali.
Madaktari
wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na
wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya
dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware
anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno
hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana
na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika
taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37
lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya
ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na
28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa
kuwa na meno 32.
Baba mzazi
wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa
akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza
kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.
Habari na BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment