Karibuni tujifunze kupika pilau.

Mahitaji:
· Mchele kilo 2
· Nyama ya mfupa kilo 2
· Vitunguu maji 2 na karoti kubwa 2
· Viungo vya pilau vilivyosagwa pakiti moja(saizi ya kati)
· Viungo vya pilau visivyosagwa
· Chumvi kiasi
· Mafuta ya olive
· Njegere glasi
· Viazi ulaya nusu kilo
· Vitunguu swaum
Hatua:
Chemsha nyama yako mpaka iive, uwe umeweka chumvi kiasi, hakikisha nyama ina supu ya kutosha wakati wa kuichemsha
Osha mchele wako tayari kwa kuutumia na kisha utenge pembeni
Weka
sufuria jikoni, kisha ongeza mafuta. Yakisha pata moto weka vitunguu
maji vilivyokatwakatwa na kuaanga viive. Ongeza chumvi kiasi na endelea
kukoroga
Ongeza vitunguu swaumu vilivyopondwa na endelea kukoroga, koroga mpaka vitunguu vigeuke kuwa rangi ya kahawia na kuiva
- Ongeza viazi ulaya, vilivyomenywa na kukatwakatwa kwa ukubwa uupendao, endelea kukoroga ili vipate kuiva
Ongeza njegere na endelea kukoroga ili vipate kuiva
Ongeza
vipande vya nyama iliyochemka vyema ndani ya mchanganyiko wako. Koroga
mchanganyiko huo na acha kwa dakika chache uive vyema
Na hivi ndo itakavoonekana baada ya dakika kama 10 hivi ulizoacha mchanganyiko uive vyema
Supu
uliyochemshia nyama itakua inaonekana hivi baada ya kuondoa nyama.
Yaonekana tamu kunyweka ila usiinywe inahusika sana kwenye pishi letu
Sasa
ndo tunaanza kuweka viungo vya pilau na tunaanza na vile ambavyo
havijatwangwa. Anza na iliki huku unaongeza maji pale yanapokauka
Ongeza
viungo vingine naongelea abdalasini, weka pakiti zima (saizi ya kati),
weka binzari nyembamba pia na koroga ili vichanganyike vyema. Lazma
harufu nzuri utaisikia maana mchanganyiko wa viungo hivi una harufu tamu
mnoo
Ongeza ile supu tuliyoiweka kando ndani ya mchanganyiko huo
Sasa ongeza viungo vilivyosagwa ndani ya supu na mchanganyiko wako
Acha mchanganyiko uweze kuchanganyiko vyema huku vikichemka kwa dakika kadhaa na hivi ndo itakavoonekana
Sasa chukua ule mchele wako ulioukosha na weka ndani ya sufuria yako , koroga kidogo kisha acha uweze kuiva
Baada
ya dakika kama 5 angalia chakula chako, kumbuka kupunguza moto pale
maji yanapoanza kukauka. Angalia wali kama umeanza kuiva na kama bado
haujaiva na maji yamepungua basi ongeza maji huku unaacha viweze kuiva
vyema
Hivi ndio itakavyoonekana pale pilau yako itakapoanza kuiva vyema. endelea kupunguza moto kwani tayari menyu inakaribia kuiva
Raha
ya kula pilau na ili inoge vyema kachumbari lazima iwepo. Kuna namna
nyingi ya kuzitengeneza ila mie binafsi napenda yenye vitunguu maji,
nyanya, ndimu na chumvi baasi. Na hivi ndio kachumbari yangu ilionekana
Pakua pilau yako tayari kwa kuliwa na wageni, familia, rafiq zako. Sisi ya kwetu ilionekana hivi baada ya kupakua
Kuwa na muda mzuri kwa kujipatia maanjumati ya ukweli.....
0 comments:
Post a Comment